Wafuasi watano wa dhehebu moja
nchini Benin wamekufa kwa moshi wa mkaa, baada ya kuambiwa na
kiongozi wao kuwasha moto katika chumba kilichofungwa wakiomba
kungojea mwisho wa dunia.
Waumini kadhaa wa wamekimbizwa
hospitali baada ya tukio hilo la mwishoni mwa wiki lililotokea katika
mji wa Ajarra, karibu na Mji wa Porto Novo.
Waumini hao wa Kanisa Takatifu Mno
la Yesu Kristo, kanisa lao limekuwa likiipinga dini ya Voodoo ambayo
ndio dini kubwa kwa waumini wengi nchini Benin.
Waumini wa kanisa hilo lenye utata
wamekuwa wakipambana na waumini wa madhehebu mengine nchini Benin.
Waumini wa Voodoo wakiwa katika maadhimisho ya siku ya imani yao
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni