
Sikinde'.
Onyesho
hilo, ambalo limelenga kuwakumbusha mashabiki nyimbo za zamani za bendi
hiyo na mpya, linatarajiwa kufanyika Novemba 27, mwaka huu, kwenye
ukumbi wa DDC Kariakoo, Dar es Salaam.
Akizungumza
mjini Dar es Salaam, jana, Mratibu wa onyesho hilo, Rashid Zahor,
alisema maandalizi yote muhimu yanakwenda vizuri, ikiwa ni pamoja na
bendi hiyo kuzifanyia mazoezi ya nguvu baadhi ya nyimbo za zamani.
"Hili
ni onyesho maalumu kwa watu maalumu, ndio sababu tumelipa jina la 'Usiku
wa Sikinde', kwa sababu tunataka kuwakumbusha mashabiki, zile enzi
bendi ilipokuwa ikitamba kwa miondoko hiyo,"alisema Zahor.
Alizitaja
baadhi ya nyimbo adimu zitakazopigwa kuwa ni pamoja na Celina, Maudhi,
Taraka rejea, Clara, Christina Bundala, Hiba, Barua kutoka kwa mama,
Chenga ya mwili, Dua la kuku, Sitokubali kuwa mtumwa, Mtoto akililia
wembe, Cenjesta, Epuka jambo lisilokuhusu na nyinginezo.

Nyimbo hizo ni Jinamizi la Talaka, Za mkwezi mbili, Nikipata nitalipa,
Kibogoyo, Dole gumba, Ng'ombe haelemewi, Nundu, Tabasamu, Supu umeitia nazi na Wali nazi.Kwa
mujibu wa Zahor, wakati wa onyesho hilo, mashabiki wataruhusiwa kuomba
nyimbo watakazotaka kupigiwa na pia kutatolewa zawadi mbalimbali kwa
watakaovutia kwa mavazi na kujimwayamwaya vizuri.
Mratibu
huyo alisema onyesho hilo limedhaminiwa na Kampuni ya Isere Sports,
inayojihusisha na uuzaji wa vifaa mbalimbali vya michezo, gazeti la
Burudani na kituo cha Redio Uhuru.Kwa
upande wake, kiongozi wa bendi hiyo, Abdalla Hemba, aliwahakikishia
mashabiki kwamba, watapata burudani murua na adimu, ambayo hawataisahau
katika maisha yao.
Alisema
wameshaanza kuzifanyia mazoezi baadhi ya nyimbo za zamani ili kuwapa
mashabiki ladha halisi na kwamba, hakutakuwa na tofauti
licha ya wanamuziki wengi wa zamani kutokuwepo kwenye bendi hiyo kwa sasa. Hemba
amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi kwenye onyesho hilo ili
kuiunga mkono bendi yao, ambayo imekuwa mstari wa mbele kukuza na
kuendeleza muziki wa dansi wa miondoko ya asili.
Aidha,
kiongozi huyo wa Sikinde alisema watalitumia onyesho hilo kumkaribisha
tena jukwaani mwimbaji nyota nchini, Hassan Bicthuka, ambaye alipumzika
kutokana na kuwa mgonjwa.
Mlimani
Park Orchestra ilianzishwa 1978 na lililokuwa Shirika la Usafiri na
Huduma za Taksi (TTTS), kwa lengo la kutoa burudani kwa mashabiki.
Shirika hili lilikuwa mali ya serikali.TTTS
iliacha kuiendesha bendi hiyo mwaka 1982, ikachukuliwa na Shirika la
Uchumi na Maendeleo la Mkoa wa Dar es Salaam (DDC). Kuanzia wakati huo,
bendi ilibadilishwa jina la kuitwa DDC Mlimani Park Orchestra.
Mwaka
2010, uongozi wa DDC uliamua kujitoa kuiendesha bendi hii na kukabidhi
vyombo kwa wanamuziki ili waweze kujiendesha. Tangu wakati huo, bendi
hii imekuwa ikiendeshwa na wanamuziki wenyewe na kuchagua viongozi kila
baada ya miaka miwili.
Baadhi
ya wanamuziki waliowahi kuiongoza bendi hii ni marehemu Michael Enock,
Muhidin Gurumo, Bennovilla Anthony, marehemu Nasir Lubua, Shabani Dede,
Hussein Jumbe, Habibu Abbas 'Jeff' na Hemba.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni