TIRA:WANANCHI KATENI BIMA YA KILIMO


Wakwanza kushoto (mwenye miwani) Meneja wa TIRA Kanda ya Kaskazini Eliezer Rweikiza akiwa watumishi wengine kutoka Mamlaka hiyo wakitoa elimu kwa wageni waliotembelea banda hilo katika maonyesho ya nanenane Jijini Arusha. 
Mmoja wawaliotembelea banda la TIRA akiuliza swali kwa watumishi wa Mamlaka ya Bima nchini katika maonyesho ya nanenane Jijini Arusha. 


Na. Vero Ignatus Arusha. 


Wito umetolewa kwa wananchi kukata Bima ya kilimo ili iwasaidie wakati wa majanga.


Meneja Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Nchini (TIRA) Kanda ya kaskazini  Eliezer Rweikiza amesema kuwa mamlaka hiyo inatimiza azma ya serikali ya kuhakikisha kilimo kinasimama, kinachangia pato la Taifa, kunakua pamoja na kuwasaidia wananchi


Amesema Serikali inafanya jitihada nyingi kuhakikisha kilimo kinapata bima, hivyo kupitia ofisi ya Kamishna mkuu wa bima nchini hatua nyingi zimefanyika ikiwemo sera ya bima ya taifa inayozungumzia maswala ya kilimo kwa ujumla, sheria zilizotungwa kuielezea huduma hiyo. 


Hivyo mwanachi asiwe na wasiwasi kuhusiana na bima hii kwani uhusika wetu kwenye makampuni yanayotoa Bima iwe ni ya kilimo, Afya, mali au ya maisha lazima tusadajili sisi na kujua utendaji wao, huduma wanazozitoa niyo sababu tupo karibu yao”Alisema Rweikiza.
 
Amesema Bima hiyo ipo mahususi kwa watu wanaojihusisha na kilimo ambayo inakinga majanga yanayotokana na shughuli za  kilimo.


” Majanga haya yanatofautiana kutoka eneo moja kwenda nyingine, majanga ya mvua nyingi, mabadiliko ya hali ya hewa, mafuriko, tetemeko la ardhi, na majanga yanayohusiana na wizi shambani hivi vyote ukiwa na bima hii unaweza ukapata fidia. “alisema.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni