Mahakama mjini Moshi yaelezwa Mazito jinsi Mwanafunzi wa shule ya Scolastika alivyouawa kinyama


Washatakiwa watatu wa kesi ya mauji ya kukusudia ya mwanafunzi wa shule ya sekondari Scolastica iliyopo katika mji wa himo ,nje kidogo ya mji Moshi Humphrey makundi wamefikishwa kwa mara ya kwanza katika mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Moshi.
Washatakiwa waliofikishwa mahakamani wakikabiliwa na shtaka la mauji hayo ni Mmiliki na Mkurugenzi wa shule ya sekondari ya Scolastica Edward Shayo,mlinzi wa shule hiyo Hamisi Chacha na mwalimu wa nidhamu,Laban Nabiswa.
Kesi hiyo namba 48 ya mwaka 2018,inasikilizwa na jaji haruna songoro ambaye amewahi kuwa jaji wa mahakama kuu,Divisheni ya biashara.
Akisoma maelezo ya kosa Wakili mkuu wa serikali,Joseph Pande alidai washatakiwa hao kwa pamoja walitenda kosa hilo Novemba 11 mwaka 2017,huku wakijua kwamba ni kinyume na kifungu cha 196 cha kanuni ya adhabu,sura ya 16 ya sheria iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002.
Kwamba Mshtakiwa wa kwanza Hamisi Chacha alimpiga kwa ubapa wa panga kichwani marehemu Humphrey na kudondoka chini huku wakirudia mara nyingi na baada ya kitendo hicho aliwajulisha mshtakiwa wa pili Edward Shayo na mshatakiwa wa tatu Laban Nabiswa.
Wakili pande amedai kwamba baada ya tukio hilo wshatakiwa wote kwa pamoja walikubaliana kuutupa mwili wa mwanafunzi huyo katika mto ghona umbali wa mita 300 kutoka ulipo ukuta wa uzio wa shule hiyo.
Katika kesi hiyo ,Jaji Songoro alisema tarehe rasmi ya kuanza kwa kesi hiyo itapangwa na msajili wa mahakama kuu na pande zote zitajulishwa lakini washtakiwa watendelea kukaa rumande hadi hapo kesi yao itakapomaliza kusikilizwa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni