KAMATI YA USHIRIKI WA WATANZANIA KATIKA SEKTA YA MADINI YAANZA KUPITIA MIPANGO YA KAMPUNI ZILIZOOMBA LESENI ZA MADINI


Leo tarehe 02 Agosti, 2018 Kamati ya Ushiriki wa Watanzania katika Sekta ya Madini (Local Content) imekutana jijini Dodomakwa ajili ya kupitia mipango ya ushiriki wa watanzania katika sekta ya madini iliyowasilishwa na kampuni za uchimbaji wa madini nchini zilizoomba leseni za madini.
PICHA NA 2 (1)
Kutoka kushoto Mkurugenzi wa Idara ya Leseni na TEHAMA kutoka Tume ya Madini, Terence Ngole, Mkurugenzi wa Idara ya Sheria kutoka Wizara ya Madini, Edwin Igenge na Kamishna wa Kazi kutoka  Ofisi ya  Waziri Mkuu ( Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu), Hilda Kabissa wakifuatilia ufafanuzi uliokuwa unatolewa na Mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye ni Kamishna- Tume ya Madini, Dk. Athanas Macheyeki (hayupo pichani).
PICHA NA 4 (2)
Kamishna wa Kazi kutoka  Ofisi ya  Waziri Mkuu ( Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu), Hilda Kabissa akiwasilisha mchango wake kwenye kikao hicho.
PICHA NA 5 (1)
Meneja wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu kutoka Tume ya Madini, Miriam Mbaga akieleza jambo kwenye kikao hicho.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni