Rais wa Marekani Donald Trump 
amezionya kampuni za mawasiliano ya mtandao Google, Twitter na Facebook 
na kusema kuwa ataichukulia hatua kutokana na  kile alichokiita kuminya 
taarifa zake na za mrengo wa kihafidhina.
Licha ya Rais Trump hajabainisha ni hatua gani hasa ambazo utawala wake unapanga kuzichukua.
Trump ameitaka mitandao hiyo kuwa 
makini baada ya awali kuishutumu Google kwa kupindua matokeo ya taarifa 
pale mtumiaji wa mtandao huo anapotafuta habari kumhusu Trump.
Hata hivyo, Google wamekanusha shutuma kuwa mtandao wao unaupendeleo na kusema hawafungamani na itikadi yoyote ya kisiasa.
Chanzo:BBC Swahili.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni