PM AMTAKA KAMANDA WA TAKUKURU KUMKAMATA MTENDAJI WA KIJIJI ALIKULA FEDHA ZA WANANCHI


PMO_0219
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Nzega kwenye ukumbi wa halmashauri hiyo Agosti 17, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PMO_0308
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Bukene Selemani Zedi katika mkutano wa hadhara aliouhutubia kwenye Uwanja wa Taifa  wa Bukene Agosti 17, 2018. Katikati ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Tabora, Hassan Kasubi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PMO_0333
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia  mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Taifa  wa Bukene wilayani Nzega, Agosti 17, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PMO_0267
Wananchi wa Bukene wilayani Nzega wakimshangilia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Taifa  wa Bukene kuhutubia mkutano wa hadhara Agosti 17, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
NA TIGANYA VINCENT
17 August 2018
TABORA
SERIKALI imemwagiza Kamanda ya Kikosi cha Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) wilayani Igunga kumtafuta na kumukamata Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Bulangamilwa kwa tuhuma za kula shilingi milioni 140 za wanakijiji.
Agizo hilo lilitolewa jana na Waziri Mkuu  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa wakati akizungumza  na Watumishi wa umma wa Halmashauri na Wilaya ya Igunga baada ya Mbunge wa Jimbo la Manonga Seif Gulamali kulalamika kuwa Mtendaji huyo licha kula fedha hizo ilishia kuhamisha kwenda sehemu nyingine.
Mhe. Majaliwa alisema haiwezekani wananchi wanajitahidi kujiwekea fedha kwa ajili ya maendeleo yao ya kijiji kisha anatokea mtu mmoja anakula fedha zao.
Alisema vitendo vya aina hiyo vinawakatisha tamaa watu ambao wanaojitolea kuchangia fedha kwa ajili ya shughuli za maendeleo yao.
Waziri Mkuu alisema Serikali ya Awamu ya Tano haiwavumili watumishi ambao wezi, wavivu na wala rushwa nainapotekea inachukua hatua haraka.
Awali akitoa salamu za Jimbo lake Gulamali alisema katika kipindi cha miaka nyuma Kijiji cha Bulangamilwa kilipata shilingi milioni 140 zilizotokana na shughuli za uchimbaji wa madini katika eneo hilo lakini ziliishia mfukoni mwa Mtendaji wa Kijiji ambaye baadaye alihamishwa.
Alisema wananchi walijaribu kufuatilia fedha zao hawakuweza kupata majibu jambo lililowakatisha tamaa katika kushiriki kwenye uchangiaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Katika hatua nyingine Waziri Mkuu amemwagiza Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Igunga kuwatafuta na kuwakamata watu wote  waliopewa fedha za  ununuzi wa mashine ya kukoboa mpunga katika Kijiji cha Choma ambayo hadi hivi sasa haijulikana ilipo.
Alisema mashine hiyo ambayo ilikuwa inunuliwe kwa gharama za shilingi milioni 35 ingesaidia kuinua hali ya mapato ya kijiji kama ingekuwa imefungwa.
Waziri Mkuu alisema haiwezekani wananchi wajitoe kwa ajili ya kuanzisha mradi fulani lakini matokeo yake fedha zinaishia mifukoni mwa wachache.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni