Ifike mahali turuhusu mtu akihama chama ahame na ubunge wake – Nape Nnauye


Mbunge wa jimbo la Mtama tiketi ya CCM, Nape Nnauye amefunguka kuzungumzia hama hama ya wabunge na madiwani wengi kutoka nyama vya upinzani kwenda chama tawala cha CCM.

Malalamiko ya wengi katika mitandao ya kijamii yanadai kwamba hama hama hiyo imeweza kuisababishia serikali gharama kubwa za kurudia uchaguzi.
Akiongea na Azam TV Ijumaa hii, Mhe Nape amedai ingawa ni jambo gumu lakini angependa wabunge ambao wanahama vyama waruhusiwe kuendelea na nafasi zao kwa kuwa wamechaguliwa na wananchi.
“Hii kitu nadhani ina ukakasi, najua haivunji sheria lakini ina ukakasi na kama ina ukakasi nadhani umefika wakati pengine tukatengeneza forum ya kupitia sheria zinazoongoza huu mchezo kwenye mfumo wa vyama vingi,”
“Kwa mfano ifike mahali turuhusu mtu akihama, ahame na ubunge wake”
Wiki iliyopita tulishuhudia mbunge wa Ukonga Mwita Waitara akihama CUF na kuhamia CCM na wiki hii kamati kuu ya chama hicho imempitisha kugombea ubunge.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni