OMAR AL-BASHIR ATEULIWA TENA KUGOMBEA URAIS SUDANI


BASHIR
Rais wa Sudan Omar al- Bashir.
Chama tawala nchini Sudani kimemteua kwa mara nyingine tena Rais wa sasa, Omar al-Bashir kuwa mgombea wa kiti cha urais kwenye uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwaka 2020.
Shirika la habari la AFP limeripoti kwamba, Bashir aliteuliwa katika mkutano wa chama tawala uliofanyika mjini Khartoum siku ya Alhamisi.
Rais Bashir amekuwa akiiongoza Sudan tangu mwaka 1989 baada ya kuchukua madaraka katika mageuzi ya kijeshi na ameshiriki mara mbili kwenye uchaguzi wa kinyang’anyiro cha urais tangu katiba mpya ya nchi hiyo ilivyopitishwa mwaka 2010.
 Bashir alishinda uchaguzi wa mwaka 2010 na 2015 na amekuwa madarakani kwa takriban miaka 30, aliwahi kusema siku za nyuma kuwa angeachia madaraka ifikapo mwaka 2020, na alikuwa hajaweka wazi dhamiri yake ya kugombania tena.
Wachambuzi wa kisiasa wanasema kwa kuwa katiba ya Sudan inaruhusu mihula miwili ya miaka mitano kila mmoja, Bashir ataweza kugombea tu baada ya kubadilisha katiba.
Chanzo: V.O.A Swahili

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni