Mkuu wa Wilaya ya
Arumeru mkoani Arusha, Mh. Jerry Muro amefungua mkutano wa wabobezi wa
utafiti katika ukanda wa Africa Mashariki ” The Eastern Africa Research
and Innovation Management Association, Tanzania Chapter, mapema hii leo.
Dc Muro
amemuwakilisha Mkuu wa mkoa wa Arusha. Mh. Mrisho Mashaka Gambo Mkuu wa
Wilaya amewapongeza Watafiti kwa Ubunifu wa kuwa na Jukwaa la Pamoja
kutafuta suluhisho la changamoto zinazowakabiri wananchi wa jumuia ya
Africa ya Mashariki.
Pia amewaeleza juhudi
mbali mbali ambazo zinafanywa na Serikali yaTanzania za kuwezesha
taasisi za kitafiti na za Elimu ya juu katika utafiti.
Ameeleza kuwa
serikali inasubiria kupata mrejesho juu ya changamoto mbali mbali
zitakazo bainishwa na wataalam hao ili kuendelea kutoa ushirikiano
stahiki katika kuzifanyia kazi changamoto hizo Dc Jerry Muro,
ameipongeza Taasisi ya Sayansi na Technolojia ya Nelson Mandela, iliyoko
Tengeru, Arusha kwa kuonesha mfano mzuri wa tafiti zinazogusa maisha ya
watu na viwanda na kusema kuwa kazi kubwa iliyobakia ni kushirikiana
katika kuzifikisha kwa jamii na viwanda.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni