Katika hali ya kushangaza gari la Ikulu ya Rais Uhuru Kenyatta aina ya Nissan Patroll V8 black limekamatwa mjini Bomang’ombe wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro.
Kwa mujibu wa RPC Kilimanjaro watu watatu wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano zaidi.
Source: azam TV
=======
Jeshi la polisi linawashikilia watu wawili wakazi wa Moshi kwa kukutwa na gari inayosadikiwa kumilikiwa na Ikulu ya Nairobi nchini Kenya ambayo inasadikiwa kuibwa nchini Kenya tarehe 19 Agosti.
Gari aina ya Nissan V8 yenye Namba za Usajili KCP 184 RV. Lakini ilikuwa imebandikwa T954 DEQ ilikamatwa ikiwa njiani ikielekea Kilimanjaro ikitokea nchini Kenya. Imekamatwa kwenye belia ya Msomali Boma ng’ombe. Tarehe 19 kulikuwa na taarifa ya gari aina ya V8 kuibiwa Kenya na gari ndo hii.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni