Serikali imewaasa Watanzania kuacha Tabia ya Kusema maneno yaasiyo ya kweli na majungu yanayowakatisha tamaa wawekezaji wazalendo na kushindwa kuendelea na shughuli za uwekezaji nchini pamoja na kuwasababishia hasara kubwa.
Aidha imesema wachimbani wadogo wa ndani wanaofuata sheria za uchimbaji madini waungwe mkono ili na wao wakue na kufikia daraja wachimbaji wakubwa, kama ilivyo migodi mikubwa.
Hayo yalielezwa na Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko , wilayani Same,mkoani Kilimanjaro wakati akikagua shughuli za uchimbaji wa madini ya Bauxite,unaofanywa na wawekezaji wa Kitanzania.
” hivi kwa nini sisi watanzania hatufurahii vitu vinavyofanywa na ndugu zetu, huyu ni Mtanzania mwenzetu amewekeza hapa anatupatia ajira, lkn kumekuwa na maneno mengi yanazunguzwa juu yake kumkatisha tamaa na wakati mwingine anasimamisha shughuli za uchimbaji kupisha uchunguzi wa kile kinachozungumzwa, zaidi ya Tume 7 zimeundwa kwa nyakati tofauti matokeo yake uchunguzi unaonesha hakuna ukweli wa kinachosemwa, hii tabia sio nzuri, tuwaunge mkono wasonge mbele kwa manufaa yetu na taifa kwa jumla”, Alisisitiza Doto.
Sambamba na hilo, ametoa wito kwa Halmashauri zote nchini pamoja na Serikali za mitaa, kuweka utaratibu mzuri wa kutoza kodi zinazotokana na shughuli za uchimbaji madini katika maeneo yao na tozo hizo ziwekwe kisheria ili kuepusha mkanganyiko uliopo sasa ambapo kila halmashauri inatoza kwa kiwango chake, tofauti na ile iliyowekwa katika sheria ya madini ya mwaka 2010 na kufanyiwa marekebisho 2017.
Alifafanua kwa sasa kila halmashauri au Serikali ya mitaa zimekuwa zikitoza kiwango cha fedha kulingana na wao wanavyoona inafaa,kitu ambavyo kinawaumiza wachimbaji wadogo kutokana na kuwepo kwa kodi nyingi katika shughuli zao za uchimbaji wa madini.
Alisema hali hiyo pia inasababisha Wachimbaji wadogo kutokufuata sheria za madini katikati kukwepa kulipa tozo na kodi mbalimbali zinazostahiki kwa kutorosha madini hayo, au kupitisha katika njia zisizo sahihi ili kukwepa kodi.
Akizungumzia wachimbaji wadogo, Dotto alisema, kwa serikali imeweka mazingira rafiki ya kuwawezesha wachimbaji hao kukuwa kutoka wachimbaji wadogo hadi kufikia kuwa wachimbaji wakubwa, Lengo likiwa ni kuendelea kuimarisha sekta ya madini iweze kuwanufaisha wachimbaji wenyewe na kuongeza mapato kwa Serikali na taifa kwa jumla.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Senyamule, alimuhakikishia Naibu Waziri Biteko,kuwa kwa kushirikiana na halmashauri zingine nchini wataweka viwango stahiki na vinavyolingana kutokana madini yanayopatikana katika maeneo yao ili kuunga mkono shughuli za uchimbaji wa madini hasa kukuza wachimbaji wadogo.
Aidha alisema anaimani kuwa migogoro midogo midogo inayojitokeza katika maeneo ya wachimbaji itakwisha.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni