Waziri
wa Madini akiteta jambo wakati alipotembelea mgodi wa Franone Mining & Gems
Co. Ltd uliopo ndani ya ukuta unaozunguka migodi ya tanzanite, Mirerani.
Waziri wa Madini Angellah Kairuki
amesema Serikali itaaendelea kusimamia
ulinzi na kudhibiti utoroshaji wa madini ya Tanzanite na watakaokwenda kinyume na matakwa ya Sheria, kiama chao kinakuja.
Waziri
Kairuki aliyasema hayo tarehe 1 Agosti wakati wa ziara yake mkoani Manyara
wakati alipotembelea migodi mbalimbali ya madini ya tanzanite ndani ya ukuta wa Mirerani.
Alisema
ziara hiyo ililenga kuangalia suala zima la ulinzi katika ukuta unaozunguka
migodi ya tanzanite, shughuli za uchimbaji madini mengine
zinavyofanyika na kuangalia namna uzalishaji wa madini ya tanzanite
unavyoendelea katika migodi husika.
Kairuki
aliongeza kuwa, ziara hiyo ililenga
kuangalia namna Sheria ya Madini inavyotekelezwa, masuala ya Mikataba ya
watumishi katika migodi na namna migodi
husika inavyolipa kodi mbalimbali za Serikali yakiwemo masuala ya usalama sehemu za kazi
na wafanyakazi kwa ujumla.
“Utoroshaji
madini hausaidii, fedha ni za haraka lakini zinawaadhibu watanzania walio wengi
kwa kuwa, fedha hizo hizo zingeweza kutumika katika miradi mingine ya maendeleo.
Hivyo, kila mtanzania awe mlizi wa mwenzake,” alisema Kairuki.
Awali,
akizungumza katika eneo Lemshuku
kunakofanyika shughuli za uchimbaji wa madini ya Green Garnet, waziri Kairuki alisema kuwa, serikali inatambua
mchango wa wachimbaji wadogo katika kuchangia pato la taifa kupitia shughuli za
uchimbaji, hivyo akawaasa wachimbaji nchini kufuata Sheria, kanuni na taratibu
ili kufanya shughuli halali ikiwemo kulipa kodi stahiki.
Akizungmzia
suala la ruzuku kwa wachimbaji wadogo, waziri Kairuki alisema hivi sasa
serikali imesitisha kwa muda utoaji rukuzu kwa kuwa inaandaa utaratibu wa wazi
na endelevu ambao utawezesha wachimbaji na
serikali kunufaika kupitia rasilimali madini.
Aliongeza
kuwa, serikali inaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa shughuli za uchimbaji
mdogo wa madini ikiwemo kuhakikisha kuwa inawawezesha wachimbaji kutoka
uchimbaji mdogo kwenda katika uchimbaji wa kati na kuongeza, “ tayari tumetenga
maeneo zaidi ya 44 kwa ajili ya wachimbaji wadogo.
Akitolea
ufafanuzi suala la vibarua katika migodi ya madini, aliwataka wale wote
wanaofanya vibarua katika maeneo hayo kuhakikisha kuwa, wanapata mikataba yao kabla
ya kuanza kazi.
Kuhusu
masuala ya utoaji leseni za uchimbaji madini, Waziri Kairuki alisema
ndani ya kipindi cha wiki 2 Tume ya Madini itaanza kutoa leseni kwa
waombaji waliokidhi vigezo na kuongeza kuwa, kwa wanaomiliki leseni bila
kuziendeleza watanyang’nywa na hivyo akawaasa wamiliki wasiokuwa na uwezo wa
kuendeleza maeneo yao kutoa tarifa ili waweze kuunganishwa na wenye uwezo wa
kuwekeza waweze kushirikiana.
Pia,
waziri Kairuki alihamasisha kuhusu uwekezaji katika mashine za kukata na
kunga’risha madini ili kuwezesha shughuli hizo kufanyika nchini na kuongeza
kuwa, kupitia Sheria Mpya ya Madini hairuhusu yoyote kusafirisha madini ghafi nje
ya nchi.
Kwa
upande wake, Kamishna wa Madini,
Mhandisi David Mlabwa, alisema ni lazima
Sheria, Kanuni na taratibu zizingatiwe wakati wa utekelezaji shughuli za
uchimbaji madini na kuongeza kuwa, serikali inatambua mchango wa kila aina ya
madini yanayopatikana nchini.
Naye,
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, Tumaini Magesa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya
Kiteto alisema kuwa, shughuli za uchimbaji katika eneo la Mirerani zinaendelea
na hivyo serikali itaendelea kuboresha ulinzi na kuhakikisha kwamba unaimalika.
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni