DK.KIGWANGALLA AFUNGA MOCHWARI YA HOSPITALI YA TUMBI, AIPA MASAA 72

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla ametoa siku tatu kwa uongozi wa Hospitali y teule ya rufaa ya Mkoa wa Pwani-Tumbi kufunga chumba cha kuhifadhi maiti (Mochwari) baada ya kubaini matatizo mbalimbali baada ya kufanya ziara katika hospitali hiyo.

Katika ziara hiyo, Dk. Kigwangalla alibaini mambo mbalimbali kutoenda sawa ikiwemo suala la utendaji mbovu ambapo alitoa agizo la kumtaka Mkurugenzi wa Shirika la Elimu Kibaha wanaosimamia Hospitali hiyo kutoa maelezo ndani ya masaa 24 kama anafaa kubaki ama la!.

Aidha, Dk. Kigwangalla amebainisha kuwa, hali aliyoikuta katika chumba cha kuhifadhia maiti ni mbaya hivyo ilikuondoa matatizo amelazimika kuifunga kwa muda huo wa siku tatu ilikufanyia marekebisho kwa baadhi ya mambo ndani ya chumba hicho cha mochwari hospitalini hapo.

Awali vyombo vya habari vilitoa taarifa mbalimbali juu ya Mochwari hiyo ikiwemo badhi ya maiti kuhifadhiwa nje na kuatarisha afya za wananchi.
tumbi99
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati) akiwa na uongozi wa Hospitali hiyo akiwemo Mganga Mkuu wa Hospitali, Dk. Peter Datani (kulia) akitembelea katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Pwani-Tumbi wakati wa ziara hiyo mapema jana Machi 10.2016.
tumbi hjjh
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akikagua Mochwari ya Hospitali ya Rufaa ya Tumbi.
tumbi uu
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akikagua Mochwari hiyo. Ambapo hadi sasa licha ya matatizo inayoikabili mochwari hiyo haina umeme na vifaa muhimu ikiwemo kipima cha kupimia joto kuharibika.
tumbi mochwariNaibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiangalia kifaa maalum ndani ya Mochwari hiyo ambapo hata hivyo hakifanyi kazi.
tumbi jkl
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akitoa agizo hilo kwa uongozi wa Hospitali hiyo pamoja na viongozi wa Serikali juu ya kuifunga Mochwari hiyo kwa siku tatu hadi hapo itakapofanyia ukarabati mambo mbalimbali yanayoikabili Mochwari hiyo.
tumbi hjj
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla alipowasilia kwenye Mochwari hiyo wakati wa ukaguzi huo katika Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Pwani-Tumbi, mapema jana Machi 10.2016. (Picha zote na Andrew Chale, Kibaha,Pwani).

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni