RAPA MASHUHURI ANGOLA AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA MITANO JELA

Rapa mashuhuri nchini Angola amehukumiwa kifungo cha jela miaka mitano na nusu kwa kupanga uasi dhidi ya rais Jose Eduardo dos Santos.

Rapa huyo Luaty Beirao alihukumiwa kifungo na mahakama moja Jijini Luanda, akiwa na watu wengine 16 waliofungwa kati ya miaka miwili na minane.

Watu hao 17 walikamatwa Juni wakijadili juu ya kitabu cha kuasi bila ya kufanya ghasia kwenye klabu moja ya vitabu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni