Tamasha
la Changia Damu Okoa Maisha linatarajiwa kuanza leo katika Uwanja wa
Karume, jijini Dar es Salaam ambapo pia kutakuwa na wasanii mbalimbali.
Akizungumza
na gazeti hili, Afisa Uhusiano wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili,
Aminiel Eligeisha alisema kuwa tamasha hilo litadumu kwa siku mbili
kuanzia leo na kesho na kwamba watu wajitokeze kwa wingi kuchangia damu.
Vijana wa Yamoto Band wanaoongozwa na Dogo Aslay.
“Lengo
la tamasha hili la Changia Damu Okoa Maisha ni kukusanya lita kati ya
5,000 na 6,000 ambazo ni asilimia 75 ya mahitaji ya damu katika
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili,” alisema Eligeisha.
Eligeisha
aliongeza kuwa tamasha hilo kama linavyojieleza, kwamba wachangiaji wa
damu watakuwa wanafanya hivyo ili damu hiyo ipelekwe benki ya damu kwa
ajili ya wagonjwa watakaoihitaji.
“Pia
kutakuwepo na wasanii mbalimbali watakaotumbuiza bure wakiwemo vijana
wa Yamoto Band wanaoongozwa na Dogo Aslay pamoja na wasanii kutoka
nyumba ya kuibua vipaji ‘ THT’ ambao watafanya vitu vyao wakati zoezi
hilo likiendelea,” alisema.
Tamasha
hilo limedhaminiwa na Kampuni ya Global Publishers Ltd, Clouds FM,
Pepsi Tanzania, Startimes, Abbott Fund, Benki ya CRDB, Mfuko wa Pensheni
wa GPEF pamoja na Motisun Group Tanzania Ltd.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni