(Picha na Benedict Liwenga-Maelezo)
………………………………………………………………………………………
Na. Lilian Lundo – Maelezo
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais 
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah  Kairuki 
amemsimamisha  kazi aliyekuwa mkuu wa chuo cha Utumishi wa Umma Said 
Nassoro kutokana na kushindwa kusimamia watumishi walioko chini yake
Mhe. Kairuki ametoa maamuzi hayo 
leo jijini Dar es Salaam  katika mkutano na waandishi  wa  habari katika
 moja ya kumbi zilizopo katika ofisi za Utumishi wa Umma.
“Namsimamisha Bwana Said Nassoro 
aliyekuwa mkuu wa chuo hiki kwa kushindwa kusimamia watumishi walioko 
chini yake  na kupelekea suala zima la usimamizi wa shughuli za chuo 
hususani katika matawi yake mbalimbali yaliyoko mikoani kuathirika,” 
alisema Mhe. Kairuki.
Mhe. Kairuki aliongeza kwa kusema
 kuwa usimamizi  wa Bw. Nassoro  ambao haukuwa wa ufanisi umetoa mwanya 
kwa viongozi mbalimbali wa matawi kufanya ubadhilifu wa mali za Umma 
ambapo mwaka  2011 na 2013 aliyekuwa mkurugenzi wa chuo upande wa tawi 
la Mtwara Silvanus Ngata aliongeza gharama za ujenzi.
Aidha taarifa kutoka Mkaguzi Mkuu
 wa Hesabu za Serikali (CAG) pamoja na TAKUKURU zilithibitisha 
ubadhilifu huo lakini mkuu huyo wa chuo hakuweza kuchukua hatua yoyote 
badala yake alimuhamisha Bw. Ngata kwenda kwenye tawi la Tabora na 
kuendelea na wadhifa wake.
Kutokana na ubadhilifu huo 
imempelekea Mhe. Kairuki  kumsimamisha kazi Bw. Ngata ambaye alikuwa 
Mkurugenzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma tawi la Tabora na Bw. Joseph 
Mbwiro kutokana na matumizi mabaya ya fedha za malipo ya ada kiasi cha 
shilingi bilioni moja ambazo zilikuwa zikilipwa na wanafunzi kwa mwaka 
wa fedha 2014/15.
Mhe. Kairuki ameendelea kueleza 
kuwa  bado wanaendelea kuondoa watumishi wa Umma ambao hawafuati  
 mifumo na miongozo ya Utumishi wa Umma ili kuwabakiza  watumishi ambao 
wanaonyeshe taswira nzuri na kufuata mifumo na miongozo  ya Utumishi wa 
Umma kwa ukamilifu wake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni