Baada
ya Serikali kukamilisha Ujenzi wa Darala la juu la Watembea kwa Miguu
katika Eneo la Mabatini Jijini Mwanza na kupunguza wingi wa ajali pamoja
na msongamano wa magari katika eneo hilo, Sasa juhudi zimehamia katika
eneo la Furahisha Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza ambapo pia
linajengwa Daraja la juu la Watembea kwa Miguu ili kukabiliana na foleni
katika eneo hilo ambalo limejengwa pia Kitega Uchumi cha Kisasa cha
Rock City Mall ambayo ni Mall (Soko) Kubwa katika ukanda wa Afrika
Mashariki na Kati.
Kamera ya Binagi Media Group imenasa picha za daraja hilo litakavyokuwa baada ya kukamilika hivyo enjoy kuzitamaza na uvute picha namna Mwanza inavyoendelea kuboresha miundombinu yake.
Ukifika Mwanza, Make Sure unafika Rock City Mall Mwanza.
Imeandaliwa na George Binagi-GB Pazzo @BMG.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni