Mkuu
 wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki akizungumza na waandishi wa 
habari juu ya ufunguzi wa duka la simu za mkononi na huduma za 
matengenezo ya simu Samora jijini Dar es Salaam. Wananchi wametakiwa 
kutumia simu orijio ili kuepuka usumbufu utakojitokeza kwa kuzimwa kwa 
simu feki ifikapo June mwaka huu. 
Akizungumza
 Leo jijini Dar es Salaam wakati wa uzindizi wa duka jipya la kampuni ya
 huwawei mkuu wa mkoa bwana said Meck sadiki amesema kuwa zoezi la 
uzimaji wa simu hizo uzimaji huo haujaanzia hapa nchini bali limefanyika
 katika nchi nyingi zilizoendelea.
Aidha Meck Sadick amesema kuwa ni wakati sasa wa makampuni ya simu
 kuakikisha yanatengeneza simu imara na kuwa na mafundi wa uhakika ili 
kupunguza usumbufu unaojitokeza kwa wateja wao.
 Meneja
 Huawei nchini Tanzania Peter Zhangjunliang, akizungumza na wandishi wa 
habari hawapo picha juu ya mbinu zilizotumika na kampuni ya  Huawei, 
ambapo wanajitahidi  kuwa Karibu zaidi na wateja wake na kuendeleza 
zaidi uzoefu katika matumizi ya bidhaa za Huawei. 
"Ili
 kuwahudumia Zaidi wateja wake Huawei tume fungua Maduka Mapya ya Huawei
 pamoja na huduma za matengenezo ya simu za mkononi jijin Dar es 
Salaam,baada ya kuongezeka kwa uhitaji wa bidhaa za Huawei na 
kuhakikisha kuwa na vifaa vya uhakika na orijino vinapatikana kwa wateja
 wao kirahisi.leo jijini Dar es Salaam" amesema Zhangjunliang.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadiki akipatiwa maelekezo na Meneja Huawei nchini Tanzania Peter Zhangjunliang.
 Mkuu
 wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki akikata utepe kuashiria 
uzinduzi wa  duka la simu za mkononi na huduma za matengenezo ya simu , 
Samora leo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadiki akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Huawei Tanzania.
 Mkurugenzi
 wa Mawasiliano na Teknolojia, Mh. Peter Philip akizungumza na wandishi 
wa habari hawapo pichani juu duka la kuwapatia wananchi bidhaa zenye 
viwango vya uhakika, huduma zilizo bora na pia Huawei wameweza kuenda 
sambasamba na mabadiliko ya teknolojia hivyo kuwapatia wateja wao simu 
za mkononi za kisasa,leo jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi
 wa Mawasiliano na Teknolojia, Mh. Peter Philip akiwa katika picha ya 
pamoja na uongozi wa Huawei Tanzania leo jijini Dar es Salaam. 
(Picha na Emmanuel Massaka wa Globul ya jamii).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni