Mkuu
wa Idara ya Uchumi na Uzalishaji Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Ndaro
Kulwijila (katikati), akiwakaribisha mkoani humo watafiti wa kilimo
kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), ambao walifika
ofisini kwake kujitambulisha kabla ya kwenda kutoa mafunzo kwa watafiti,
wakulima na wadau wa kilimo kuhusu matumimizi ya kilimo cha
bioteknolojia ambacho kinafanyiwa utafiti na watafiti wa kilimo kutoka
Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia ( Costech ).
Mkurugenzi
Mkuu wa Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ukiruguru kilichopo jijini
Mwanza, Dk.Evelyne Lukonge (wa pili kulia), akifurahi wakati
akisalimiana na Mtafiti Mkuu wa Jukwaa la Bioteknolojia, Dk.Emmarold
Mneney alipo wasili na maofisa wenzake watafiti katika ofisi yake
kujitambulisha kabla ya kutoa mafunzo kwa watafiti wa kituo hicho na
wadau wa kilimo. Kulia ni Mtafiti Kiongozi kutoka Costech, Dk.Nicholaus
Nyange na wa pili kushoto ni Mratibu Mkuu wa Jukwaa la Bioteknolojia
Afrika, Daniel Utunge kutoka nchini Kenya.
Mkurugenzi
Mkuu wa Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ukiruguru kilichopo jijini
Mwanza, Dk.Evelyne Lukonge, akizungumza katika mkutano huo. Kulia ni
Mtafiti Kiongozi wa Costech, Dk.Nicholaus Nyange.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni