MADHARA YA POMBE KWA WAJAWAZITO HAYANATOFAUTI NA YA VIRUSI VYA ZIKA

Wataalam wa afya wamebaini kuwa unywaji wa pombe kwa mwanamke mjamzito unaweza kuwa na madhara kwa mtoto aliyetumboni, sawa kabisa na madhara ya viruzi vya Zika kwa wajawazito.

Kwa hiyo mjamzito sasa asichukulie kuwa yupo salama kwa kutokuwapo Brazil ambako kuna maambukizi ya Zika, iwapo bado atakuwa anakunywa pombe ambayo nayo inamadhara yasiyoyakawaida kwa watoto.

Kwa mujibu wa utafiti uliochapishwa na kituo cha Kudhibiti Maradhi Kenya, Februari 4, si virusi vya Zika tu vyenye madhara ya ubongo kwa mtoto hata pombe nayo husababisha madhara kwa wajawazito.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni