Kaimu
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Pan African Energy Andy Hanna ( wa pili kutoka
 kulia) akielezea majukumu ya kampuni hiyo mbele ya Waziri wa Nishati na
 Madini Profesa Sospeter Muhongo pamoja na watendaji wa Wizara  ya 
Nishati na Madini pamoja na  Taasisi zilizopo chini yake.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akielezea fursa za uwekezaji katika sekta ya gesi nchini.
Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Pan African Energy Andy Hanna akisisitiza jambo katika kikao hicho.
Kaimu
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Pan African Energy Andy Hanna (kushoto) na 
Mwenyekiti wa Kampuni ya Pan African Energy Nchini Patrick Rutabanzibwa 
(kulia) wakinukuu maelekezo  kutoka  kwa Wiziri wa Nishati na Madini 
Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani).
Na Greyson Mwase, Dar es Salaam
Waziri
 wa  Nishati na  Madini Profesa Sospeter Muhongo amelitaka  Shirika la 
Umeme Tanzania (TANESCO) na Shirika la  Maendeleo  ya Petroli Nchini 
(TPDC) kufanya kazi katika  mtindo wa kisasa ili nishati ya umeme iweze 
kuwa  ya  uhakika kwa maendeleo  ya uchumi wa nchi.
Profesa
 Muhongo aliyasema hayo katika kikao chake na Kampuni ya Pan African 
Energy kilichofanyika jijini Dar es Salaam  kilichoshirikisha pia 
watendaji kutoka wizara ya nishati na madini, TANESCO, TPDC na Mamlaka 
ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA).
Alisema
  mahitaji ya gesi kwa ajili ya kuzalisha umeme wa uhakika ni makubwa, 
hivyo hakuna sababu  ya  kuwepo  kwa upungufu wa nishati ya umeme 
 nchini wakati kuna gesi ya uhakika.
Alifafanua
 kuwa haiwezekani shirika la TPDC likadai kuwa kuna gesi ya kutosha kwa 
ajili ya kuzalisha umeme, wakati kuna upungufu wa umeme nchini.
Alisema
  serikali ina mpango wa kuhakikisha kuwa  wananchi wote hasa waishio 
vijijini  wanaunganishwa na umeme wa uhakika kupitia Wakala wa Nishati 
Nchini (REA) hivyo ni jukumu la mashirika hayo kuhakikisha yanabuni 
miradi na kukaribisha wawekezaji mbalimbali  katika uzalishaji wa umeme 
 wa uhakika ili wananchi wote waweze kuunganishwa na huduma ya umeme.
Alisisitiza
 kuwa amekwishawaalika wawekezaji mbalimbali kwa ajili ya kuwekeza 
kwenye uzalishaji  wa  Megawati 1000 za umeme  kwa ajili ya kuingizwa 
kwenye  gridi ya  taifa, hivyo ni vyema shirika la TPDC likahakikisha   
gesi ya uhakika inapatikana ili  umeme uweze kuzalishwa mara moja.
“
  Lengo la  serikali kupitia  Wizara ya Nishati na Madini ni kuhakikisha
 kuwa ifikapo  mwaka 2025 Megawati 10,000 zinazalishwa, hivyo sekta ya 
nishati  kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi na kutoka kwenye  kundi la 
nchi masikini duniani  na kuingia kwenye kundi la nchi za  kipato cha 
kati, kama   Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, inavyofafanua,”alisema 
Profesa Muhongo.
Wakati
 huo huo, Profesa Muhongo aliitaka kampuni ya Pan Afrian Energy 
 kuhakikisha inatatua changamoto zote  inazozikabili  kwa kipindi cha 
miezi mitatu kabla ya kukutana naye  Juni 01 mwaka huu kwa ajili ya 
kupokea mapendekezo ya kampuni hiyo katika kuzalisha  gesi ya uhakika.
Alisisitiza
 kuwa kutakuwepo na utaratibu wa kukutana na kampuni hiyo kila baada ya 
miezi mitatu kwa ajili ya kujadili utendaji kazi wa kampuni hiyo, na 
serikali ipo tayari kutoa msaada pale kampuni itakapokwama.
Aidha,
 Profesa Muhongo aliitaka kampuni hiyo kuweka utaratibu wa kuajiri 
 vijana wa kitanzania wanaomaliza masomo ndani na nje  ya nchi baada ya 
kupata ufadhili kutoka serikalini.
“
 Kwa sasa tuna  vijana wengi waliohitimu mafunzo  kwa ngazi  ya shahada 
za uzamili katika masuala ya mafuta na gesi katika  vyuo mbalimbali 
ndani na nje ya nchi kama Norway, Uingereza na China, hivyo ni vyema 
 wakapata ajira katika kampuni ya  Pan African Energy, ili nao waweze 
kufaidika na elimu na uwepo wa uwekezaji katika shughuli za utafutaji na
 uchimbaji wa gesi na mafuta nchini,” alisisitiza Profesa Muhongo.
Naye
  Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Pan African Energy Andy Hanna, 
akielezea mafanikio ya uwekezaji kupitia  kampuni yake, alieleza kuwa 
kampuni hiyo imefanikiwa kutoa  ajira 87 kwa watanzania na kuboresha 
huduma  za jamii kama vile kutoa huduma ya umeme  bure katika eneo la 
Kilwa kilipo kituo chake za kuzalisha gesi.
Aliendelea
 kusema kuwa kampuni ya Pan African Energy imejenga  zahanati pamoja na 
kutoa mafunzo kwa waajiriwa wake lengo likiwa ni  kuhakikisha kuwa 
kampuni hiyo inakuwa na wataalam wazawa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni