MWENYEKITI WA SERIKALI YA MTAA AKUTWA NA SILAHA ZA KUTISHA UINGEREZA

Silaha za aina tofauti za kutisha zilizokusanywa mtu zinazofikia 500 pamoja na risasi 200,000 zimekutwa kwenye nyumba ya Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa nchini Uingereza.

Polisi walibaini silaha hizo haramu kwenye nyumba ya mwenyekiti huyo ambaye ni mwendesha crane aitwae James Arnold huko Wyverstone, Suffolk, ni shehena kubwa ya silaha kuwahi kukutwa Uingereza.

Hata hivyo miezi mitatu kupita tangu kukamatwa kwa shehena hiyo na mtuhumiwa kukamatwa, alikuja kufariki kwa ugonjwa wa saratani ya kongosho na hakuweza kushtakiwa na kutiwa hatiani.
                                     Sehemu ya shehena ya silaha hizo kama inavyoonekana 
                                                  Aina tofauti ya silaha hizo kama zinavyoonekana
                             Hii nayo ilikuwemo katika shehena ya silaha zilizokamatwa

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni