Viongozi
kutoka shirika la Ndege la Etihad wakiwa na tuzo ya shirika la Ndege la
mwaka 2016 waliyopokea kutoka jarida la Air Transport World (ATW) katika
hafla iliyofanyika nchini Singapore. Kutoka kushoto Hareb Al Muhairy,
Makamu wa Rais masuala ya kishirika na kimataifa; Karen Walker, Mhariri
mkuu wa jarida la ATW; James Hogan, Rais na Afisa mtendaji; na James
Rigney, Afisa mkuu wa Fedha.
SHIRIKA
la Ndege la Etihad limetunukiwa tuzo ya Shirika la Ndege la mwaka 2016
kutoka Jarida kubwa la Air Transport World (ATW) lililopo nchini
Marekani linaloandika habari za usafiri wa anga. Tuzo hii imelitambua
Shirika hili kwa kuwa na timu iliyo na mikakati inayohamasisha ukuaji wa
Shirika na kukuza ushikiano wake wa kipekee; katika kuleta bidhaa zenye
manufaa makubwa; kujenga nguvu kazi yenye hamasa; na kujenga utetezi wa
kidiplomasia wakati wa ugomvi mkali kati yao na wasafirishaji wa
Wamarekani.
Shirika
la Ndege la Etihad lilichaguliwa na bodi ya wahariri wa jarida hili
huku kukiwa na ushindani mkubwa kutoka kwa mashirika zaidi ya 100 kutoka
nchi mbalimbali ulimwenguni. Tuzo hii ilitolewa katika hafla ya chakula
cha jioni iliyohudhuriwa na wadau wa sekta ya usafiri wa anga. Shughuli
hii huandaliwa mara moja kila mwaka, ya mwaka huu ikiwa ya 42 tangu
kuanzishwa kwake na kufanyika usiku wa kuamkia tamasha la anga la
Singapore.
James
Hogan, Rais na Mkurugenzi Mkuu wa Etihad, alisema: “Tuzo hii ni
kiashiria cha kufikia malengo tuliyojiwekea takribani miaka 13 iliyopita
ya kuwa salama, kuwa shirika lenye faida na kuwa shirika lenye ubora wa
hali ya juu. Inaonyesha nguvu zetu - mbinu imara za biashara, bidhaa
zenye ubunifu na huduma iliyo bora zaidi inayotolewa na wafanyakazi
zaidi ya 27,000 walio na ari kubwa. Nimefurahi kupokea zawadi hii kwa
niaba yao, kama Shirika, tumejitahidi kutoa huduma za kipekee kwa
wasafiri na tumekuza biashara yetu ili kusaidia sura ya usafiri wa anga
duniani”.
Ili
kustahili hii tuzo, ATW walisema Shirika lilitakiwa kuonyesha mafanikio
ya kipekee katika operesheni zake, uwezo wa kifedha, huduma bora kwa
wateja, usalama na mahusiano bora ya wafanyakazi. Timu ya uongozi wa juu
pia ilibidi kuonyesha ubunifu na uwezo wa kuvumbua mikakati itakayoipa
kampuni muonekano tofauti na nyingine.
Karen
Walker, Mhariri Mkuu wa jarida la Air Transport World, alisema: “Shirika
la Ndege la Etihad limejitenga na wengine na linaenda katika mkondo
wake wakipekee. Tunayo furaha kusherekea mafanikio ya timu ya Etihad
katika tuzo za mwaka huu za ATW hapa Singapore. “Etihad inastahili
kupewa tuzo hii ya juu ya Shirika la Ndege la Mwaka”, alisema James
Hogan huku akisisitiza kuwa “Suala sio kuwa shirika kubwa tu bali
shirika bora zaidi”
Kwa upande wa bidhaa na huduma kwa wateja, Shirika la Ndege la Etihad
lilielezewa na ATW kuwa wabunifu, wakiweka msisitizo katika vyumba vyao
vya kipekee ndani ya Airbus A380 na Boeing 787. Pia waliiongelea
“Makazi” ambayo ni vyumba vya kwanza duniani kuwa na sehemu tatu za;
kulala, kupumzika na bafu.
Katika mahusiano ya kibiashara, ATW waliona Etihad na washirika
wametengeneza mtandao wenye faida duniani kama msingi wa mbinu zake
kibiashara. Ushirikiano wake na airberlin, Darwin Airline (iliyopo
Uswisi), Air Serbia, Alitalia, Jet Airways, Air Seychelles na Virgin
Australia umesaidia Shirika kuwapa wateja wao chaguo zaidi, uwezo wa
kujadili bei na wasambazaji, mafunzo kwa wafanyakazi na mtandao
uliosambaa zaidi ulimwenguni.
Katika mgogoro kati ya Etihad na wasafirishaji wa Marekani juu ya
vitendo visivyohamasisha ushindani; ATW walisema James Hogan na timu
yake walionyesha staha na heshima kwa kulitetea Shirika lao na mbuni
zake kwa ukweli kuliko kutumia mashambulizi. Wahariri wa ATW walimwaga
sifa kwa Etihad ambapo James Hogan alisema: “Mawe mengi yamerushwa
kwetu, lakini tumejibu kiutulivu na kwa ukweli, tulionyesha ushindani
mpya tulioleta katika soko.”
Upande wa wafanyakazi, ATW iliwaelezea Etihad kama “raia mwema”
ikilielezea nguvukazi yao kama ‘familia’ na kwa kufanyia kazi mikakati
yao ya kukuza nguvukazi yao (ikiwa na raia 3,000 wa UAE) na kuwapa kazi
kupitia programu mbalimbali. Wafanyakazi wanaungwa mkono na Maafisa
rasilimali, timu ya ustawi, wakipata huduma mbalimbali kama sehemu za
mazoezi, sehemu nzuri za malazi na chekechea kwa watoto wao.
Katika mipango endelevu, ATW iliwapongeza Etihad kwa mipango yake ya
kupunguza matumizi ya mafuta, kufanya utafiti wa nishati mbadala na
washirika wake wakuu, na kuwashughulisha wafanyakazi katika programu za
kuokoa mazingira.
Katika
mwaka 2015, Shirika la Ndege la Etihad lilizindua njia sita zaidi
katika mabara 3 na hivyo kufikisha jumla ya vituo vyake ulimwenguni
kufika 116 kwa kutumia ndege 121. Zaidi ya wageni milioni 17 wamesafiri
na Shirika hili mpaka mwaka jana, kutoka milioni 15 wa mwaka 2014.
Etihad ilizindua ndege yake mpya aina ya Boeing 787 Dreamliner – ya
kwanza kati ya 71 zilizowekwa oda.
Shirika
la Etihad lilitambuliwa na bodi ya wahariri wa ATW kwa “kuwa na ukuaji
wa haraka na uliopangwa, kutoa huduma bora na zinazofikia malengo yao na
kwa kuwa na fikra endelevu daima”. Etihad pia ilisifiwa kwa “kuwa na
uwezo mzuri kifedha, usalama na uwezo wake kubeba mizigo”
ATW ni
jarida la kimamlaka linalotoka kila mwezi na kukidhi mahitaji ya
jumuiya za wadau wa usafiri wa anga ulimwenguni. Wahariri wake
wameteuliwa kutoka kila tuzo za uandishi wa usafiri wa anga zilizopo,
wakiangalia uzoefu na utaalamu wao.
Tuzo
za mafanikio katika sekta ya anga za ATW zilianzishwa 1974 ili kutambua
umahiri katika operesheni za mashirika ya ndege duniani na kuwapa
pongezi wadau wa sekta hiyo. Jarida hili lipo Marekani na timu yake ya
wahariri imefika kote ullimwenguni.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni