IPIGIE KURA FILAMU YA MPANGO MBAYA KATIKA SHINDANO LA AMVCA 2016 ILI KULETA USHINDI TANZANIA

Wadau wa filamu nchini tunaomba muendelee kuipigia kura filamu yetu ya Mpango Mbaya ilichezwa na washiriki wachanga kabisa ambao ni zao la Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) Msimu wa Kwanza

Filamu ya Mpango Mbaya ni moja ya filamu nzuri na yenye ubora wa hali ya juu na ndio sababu kubwa iliyopelekea kuingia katika Kinyanganyiro cha African Magic Viewers Choice Awards 2016 katika kipengele cha BEST MOVIE - EAST AFRICA.



Jinsi ya Kupiga Kura tembelea tovuti hii http://amvca2016 awards.dstv.com/nominees/best-movie-east-africa_2

Na kama hauna akaunti DSTV unachotakiwa ni kujisajili kupitia kiunganishi hiki http://africamagic.dstv.com/ halafu nenda sehemu ya AMVCA halafu pigia kura kipengele cha BEST MOVIE - EAST AFRICA chagua MPANGO MBAYA hapo utakuwa umeiwezesha filamu ya MPANGO MBAYA kuisaka nafasi ya kuipeperusha bendera ya Tanzania nchini Nigeria. 


Tuendelee Kupiga Kura Ili Tulete Heshima Nyumbani ni Zamu ya FIlamu sasa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni