Rais Yoweri Museveni wa Uganda
amekanusha madai ya upinzani ya wizi wa kura katika uchaguzi mkuu
ulioisha, na kushutumu ukosoaji uliofanywa na Jumuiya ya Kimataifa.
Museveni alitangazwa mshindi wa
urais na Tume ya Uchaguzi kwa kupata asilimia 60 ya kura, akifuatiwa
na mpinzani wake mkuu, Kizza Besigye aliyepata kura asilimia 35.
Besigye medai kuibiwa kura na
kutoa wito kwa Jumuiya ya Kimataifa kutokutambua matokeo
yaliyomrejesha madarakani rais Museveni.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni