Manchester City imepata matokeo
mazuri katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya 16 bora baada
ya kuifunga Dynamo Kiev kwa mabao 3-1, kwenye mchezo wao wa awali
uliochezwa nchini Ukraine.
Katika mchezo huo Manchester City
ilitawala katika kipindi cha kwanza na Sergio Aguero alikuwa wakwanza
kutikisa nyavu za Dynamo Kiev, kabla ya David Silva naye kuongeza bao
la pili.
Mchezaji wa Kiev Vitaliy Buyalsky
alifunga bao kwa shuti lililopinda, lakini Yaya Toure alizima ndoto
ya kurejeshwa mabao hayo kwa kupachika bao la tatu mnamo dakika ya
tisini ya mchezo huo. Matokeo mengine PSV Eindhoven 0-0 Atl Madrid.
David Silva akifunga bao la pili katika mchezo huo
Yaya Toure akipiga mpira wa kuzungusha uliojaa wavuni na kuandika bao la tatu la Manchester City
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni