MASHINDANO YA LIGI YA VYUO VIKUU JIJINI MWANZA YAFIKIA TAMATI CHINI YA VODACOM TANZANIA

Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha SAUT Mwaka wa(3)jijini Mwanzani,Emanuel Simbo(kushoto)akijaribu kumtoka John Lucas wa timu ya walimu,wakati wa fainali za mashindano ya ligi ya Vyuo vikuu iliyodhaminiwa na Vodacom Tanzania na kufanyika jijini humo mwishoni mwa wiki,Ambapo timu ya walimu lililazwa kwa magoli 6-4.
Baadhi ya mashabiki wakishuhudia mtanenge wa fainali za mashindano ya ligi ya Vyuo vikuu vya jijini Mwanza yaliyodhaminiwa na Vodacom Tanzania mwishoni mwa wiki,Ambapo timu ya walimu lililazwa kwa magoli 6-4.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha SAUT jijini Mwanza,Tadeus Mukamwa(wakwanza kushoto) akimkabidhi zawadi Farida Abdallah zawadi baada ya timu yake ya Netball kuibuka mshindi wa pili wakati wa fainali za mashindano ya ligi ya Vyuo vikuu iliyodhaminiwa na Vodacom Tanzania zilizofanyika jijini Mwanza mwishoni mwa wiki.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha SAUT jijini Mwanza,Tadeus Mukamwa(wakwanza kushoto) akimkabidhi zawadi Mary Mshumbusi zawadi baada ya timu yake ya Netball kuibuka mshindi wa tatu katika fainali za mashindano ya ligi ya Vyuo vikuu iliyodhaminiwa na Vodacom Tanzania zilizofanyika jijini Mwanza mwishoni mwa wiki.
Mkuu wa Vodacom Tanzania kanda ya ziwa,Dominician Mkama(kushoto) akimvalisha medali Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha SAUT jijini Mwanza,Zuena Rajabu baada ya timu yake ya Netball kuibuka kidedea kwa magoli 13-9 wakati wa fainali za mashindano ya ligi ya Vyuo vikuu yaliyodhaminiwa na Vodacom Tanzania na kufanyika mwishoni mwa wiki jijini humo.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha SAUT jijini Mwanza,Tadeus Mukamwa(wapili kushoto) akimkabidhi Kapteni wa timu ya Wanafunzi wa Chuo hicho, Sammir Emmed Kombe la Ushindi wa mashindano ya ligi ya Vyuo vikuu iliyodhaminiwa na Vodacom Tanzania zilizofanyika jijini humo baada ya kuishinda timu ya Walimu 6-4 mwishoni mwa wiki,wengine katika picha Mhadhiri wa Chuo hicho Padri Leons Maziku(kushoto) Mkuu wa Vodacom Tanzania kanda ya ziwa,Dominician Mkama(watatu toka kushoto)
Timu ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha SAUT jijini Mwanza,wakishangialia na kombe lao baada kuibwaga timu ya walimu 6-4 na kuibuka mabingwa wa mashindano ya ligi ya Vyuo vikuu yaliyofanyika jijini Mwanza mwishoni mwa wiki na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni