Msajili wa Hazina, Bw. Lawrence Mafuru akishuka
kwenye gari wakati alipowasili kwenye mradi wa Eco Residence ulioko
Kinondoni Hananasifu unaojengwa na shirika la Nyumba la Taifa NHC huku
akiongozwa na Mkurugenzi wa shirika hilo Bw. Nehemia Mchechu tayari kwa
ukaguzi wa jengo hilo ambalo nyumba zake zote zimeshauzwa na
linatarajiwa kukabidhiwa hivi karibuni kwa Shirika hilo.
Akizungumza
na Vyombo vya habari mara baada ya ukaguzi wa jeno hilo Msajiri wa
Hazina Bw. Lawrence Mafuru amepongeza uongozi wa NHC kwa kazi kubwa
wanayoifanya ambapo wamefanikiwa kujenga majengo yenye tahami ya
shilingi Trilioni 3.5 kutoka umiliki wa mwanzo ambapo kulikuwa na
majengo yenye thamani ya shilingi trilioni 1.
Mkopo
uliotumika kugharamia ujenzi wa majengo hayo mapya kutoka mabenki
mbalimbali ni jumla ya shilingi Bilioni 300 ambazo kiasi cha shilingi
Bilioni 100 zimeshalipwa tayari katika mabenki hayo na kiasi cha
shilingi bilioni 200 zinaendelea kulipwa
Naye
Mkurugenzi wa Shirika hilo Bw. Nehemia Mchechu amesema shirika hilo
linao mpango mkubwa wa ujenzi wa nyumba 500 za gharama nafuu kwa ajili
ya watanzania wenye kipato cha chini ambazo zitaanza kujengwa mwaka huu
huko Luguruni wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam..(PICHA NA JOHN
BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
Msajili wa Hazina, Bw. Lawrence Mafuru akimsikiliza
Violet Mafuwe Msanifu wa majengo kutoka kampuni ya CPI Iternational
ambaye pia ni Meneja Mradi wa Eco Residence wakati alipokagua ujenzi wa
jengo hilo.
Msajili wa Hazina, Bw. Lawrence Mafuru akimuuliza
jambo Mkurugenzi wa NHC Bw. Nehemia Mchechu mambo mbalimbali kuhusu
miradi ya shirika hilo wakati alipokagua ujenzi wa jengo hilo.
Msajili wa Hazina, Bw. Lawrence Mafuru akisikiliza maelezo ya Mkurugenzi wa NHC Bw. Nehemia Mchechu wakati alipokagua ujenzi wa jengo hilo.
Bw. Lawrence Mafuru Msajili wa Hazina akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua ujenzi wa jengo hilo.
Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba NHC akifafanua jambo kwa waandishi wa habari mara baada ya Msajili wa Hazina kukagua mradi huo.
Bw.
Lawrence Mafuru Msajili wa Hazina akiagana na Mkurugenzi wa NHC Bw
Nehemia Mchechu mara baada ya kukagua ujenzi wa jengo hilo.
Jengo linavyoonekana kwa nje.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni