Nyota wa filamu wa Bollywood Sanjay
Dutt ameachiwa huru na kutoka gerezani katika mji wa magharibi wa
India wa Pune.
Dutt, 56, alifungwa kwa makosa ya
kukutwa na silaha zinazohusishwa tukio la milipuko ya Mumbai la mwaka
1993 lililouwa watu 257 na kujeruhi 713.
Alitiwa hatiani kwa kununua silaha
hizo kutoka kwa walipuaji, lakini alijitetea silaha hizo zilikuwa ni
za kuilinda familia yake wakati wa ghasia za Wahindu Waislam.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni