Watoto wawili raia wa Afrika Kusini
wanamshtaki muhubiri maarufu barani Afrika TB Joshua kutokana na moja
ya majengo yake kuanguka nchini Nigeria na kumuua baba yao mwaka
2014.
Baba huyo marehemu Kalambaie wa
Kalambaie alikuwa ni miongoni mwa watu 116, waliokufa katika tukio
hilo ambapo wengi walikuwa ni raia wa Afrika Kusini.
Mwaka jana 2015, mahakama Jijini
Lagos ilisema kanisa hilo linapaswa kulaumiwa kwa uzembe uliopelekea
jengo hilo la makazi kuanguka. TB Joshua na kanisa lake wamekuwa
wakikanusha kufanya kosa lolote.
Picha ya jengo hilo la makazi lililoanguka mwaka 2014 na kuuwa watu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni