PAPA FRANCIS ATEUWA MAKARDINALI WAPYA 17

Papa Francis amewatangaza makardinali 17 wapya, wakiwemo 13 ambao wanauwezo wa kushiriki kupiga kura ya kumchagua mrithi wa Papa pindi muda wake utakapoisha.

Makardinali hao wapya wa Kanisa Katoliki wengi wao wanatokea nchi zinazoendelea katika mabara ya Afrika, Asia na Latini Amerika.

Uteuzi huo uliofanyika hii leo unaonyesha kuongezeka kwa ushawishi katika Vatican wa maaskofu wa kutoka katika mataifa yanayoendelea duniani.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni