Simu ya pili iliyobadilishwa ya
Samsung Galaxy Note 7, iliyodaiwa kuwa salama na kampuni hiyo
imeungua moto nchini Marekani.
Kampuni ya Samsung ililazimika kutoa
modeli mpya ya simu hiyo baada ya kufuatia kuibuka malalamiko
yanayosababishwa na hitilafu kwenye betri.
Mwanaume mmoja wa Kentucky amesema
alihofia kufa baada ya kuamka kitandani na kuona chumba chake kimejaa
moshi.
Tukio hilo linafuatia simu nyingine
ya Galaxy Note 7 iliyobadilishwa kuwaka moto kwenye ndege ya shirika
la Southwest Airlines siku ya jumatano.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni