MATUKIO KATIKA PICHA MKUTANO WA BENKI YA DUNIA WASHINGTON DC

Wataalamu wa Masuala ya Uchumi na Fedha kutoka Tanzania wanaoshiriki Mkutano wa Mwaka wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani-IMF, wakifuatilia mazungumzo ya mkutano kati ya Shirika la Fedha Duniani-IMF na Wizara ya Fedha na Mipango, mkutano uliofanyika katika katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania, Jijini Washington DC, Marekani.
Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Kulia) wakiwa katika kikao cha kazi na uongozi wa juu wa Shirika la Fedha Duniani-IMF, ambapo masuala kadhaa yanayohusu hali ya uchumi na maendeleo ya miradi inayofadhiliwa na shirika hilo ilijadiliwa, Mkutano huo umefanyika katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania, Jijini Washington DC, Marekani.
Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dkt. Natu El-Maamry Mwamba (wa tatu kutoka kushoto) akiwa kwenye mkutano na Magavana kutoka nchi mbalimbali za kiafrika wanaoshiriki Mkutano wa Mwaka wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani-IMF, Jijini Washington DC nchini Marekani, akielezea juu ya ukuaji wa uchumi katika shughuli za mawasiliano, madini, huduma ya fedha, bima na huduma za uzalishaji wa viwandani pamoja na changamoto zilizopo..
Naibu Gavana wa Benki Kuu Dkt. Natu A. Mwamba akifafanua juu ya changamoto zinazoikumba Tanzania katika kukuza uchumi hasa katika sekta ya Elimu, Afya na Miundombinu, akiwa mmoja wa wachokoza mada wengine kutoka nchi kadhaa za Kiafrika kwenye mkutano uliojadili kuhusu hali ya Afrika, Jijini Washington DC –Marekani.

Baadhi wa wajumbe kutoka Tanzania waliohudhuria mkutano wa hali ya ukuaji wa uchumi katika Nchi za Afrika wakati Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania alipokuwa akiwasilisha mada, Jijini Washington DC-Marekani.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Dotto James akiwa na Gavana wa Benki Kuu Prof. Benno Ndullu wakibadilishana mawazo baada ya kushiriki mikutano ya siku ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani-IMF, nje ya ukumbi wa mikutano ya Benki ya Dunia Jijini Washington DC- Marekani.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni