SERIKALI YASEMA USHRIKIANO WA SAPP UNAHARAKISHA MIUNDOMBINU YA UMEME


Image result for DK KALEMANI


                          Na Mahmoud Ahmad Arusha
SERIKALI imesema kuwa ushirikiano  wan chi za umoja wa mashirika ya kuzalisha umeme kusini mwa jangwa la Sahara SAPP, unatoa msukumo  wa nchi wanachama  kuharakisha kujengwa na kukamilika kwa miundo mbinu ya mfumo wa umeme wenye gharama nafuu .
Hayo yameelezwa leo na Waziri wa Nishati Dakta Medad  Kalemani,alipokuwa akifungua mkutano wa 51 wa mashirika ya umeme ya nchi za kusini mwa afrika SAPP, na kusema kuwa lengo la mkutano huo ni kuimarisha ushirikiano uliopo ili kuwezesha nchi zote kunufaika na miundo mbinu imara ya kusafirisha umeme.
Waziri Dakta Kalemani,Tanzania, Malawi na Angola, ambazo hazijakamilisha  miundo mbinu  hiyo zinapata uzoefu ambao unawezesha kuharakisha ukamilishaji wa  miundo mbinu ya umeme na hivyo kunufaika na ushirikiano huo.
 Amesema ushirikiano huo unawezesha kuwepo na mpango madhubuti wa kuzalisha na kuuza na kununua umeme wa gharama nafuu kwa nchi wanachama.
Waziri Kalemani,amesema miradi ya umeme itawezesha kuinua na kuboresha uchumi wa nchi husika kutokana na kutekeleza miradi hiyo mikubwa ya uzalishaji umeme
Amesema mradi huo wa miundo mbinu ya umeme unaunganisha nchi wanachama ambazo ni kumi na moja na unakwenda  hadi kufikia Cairo nchini Misiri..
Waziri,amesema hivi sasa Tanzania tunazalisha umeme mwingi, katika maporomoko ya Mto Rufiji ,Somanga, pamoja na kuzinduliwa mradi wa gesi asili wa Kinyerezi na hivyo tunaweza kuuza umeme nje ya nchi na pia tunaweza kununua ueme toka nje kwa gharama nafuu zaidi .
Amesema kuwa mbali na kujiunga kwenye ushirikiano huo wa SAPP pia Tanzania imejiunga na mashirika ya umeme ya nchi wanachama wa Jumuia ya afrika mashariki lengo ni kuwezesha wananchi kupata umeme wa gharama nafuu na wa uhakika.
Amesema Tanzania sasa ina ziada ya umeme mega wati 200  baada ya kuzinduliwa kwa mradi wa gas wa Kinyerezi ,ambapo uzalishaji ni mega wati 161 1 na mahitaji ni mega wati 1537 .
Kwa upande wake mkurugenzi mtendahji wa shirika la umeme nchini ,mhandisi, Michael Tito ,amesema Tanesco imejipanga kuhakikisha umoja huo unafanya kazi kikamilifu pamoja na kuboresha miundo mbinu ya umeme ambayo itaungwanishwa kwenye gradi ya taifa.
Amesema kuwa maeneo yote ya mipakani yatapata umeme kutoka kwenye nchi wanachama kwa gharama nafuu  na hivyo kuwawezesha kuboresha maisha yao.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni