JOPO LA WATU WENYE UALBINO DUNIANI WATUA TANZANIA KUKWEA MLIMA KILIMANJARO

Jopo la watu wenye Ualibino wakiwa wameambatana na wadau wa haki za binadamu kutoka katika mataifa mbalimbali wametua katika uwanja wa ndege wa Kilimanjaro tayari kwa kukwea Mlima Kilimanjaro kuanzia leo Septemba 21,2018 lengo likiwa ni kupaza sauti juu ya changamoto za watu wenye Ualibino duniani na kuchangisha fedha za kuwawezesha baadhi ya vijana wenye Ualibino kupata elimu ya juu.

Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya Josephat Torner Foundation Europe,bwana Josephat Torner amesema lengo la safari hiyo ya kupanda Mlima Kilimanjaro yenye kauli mbiu ya “Vunja ukimya,Linda watu wenye ualbino” ni kuamsha uelewa wa jamii kuondokana na imani potofu za kishirikina juu ya watu wenye ualbino. 
Watu wenye ualbino kutoka mataifa mbalimbali wakiwasili katika uwanja wa ndege Kilimanjaro kwa ajili ya kupanda mlima Kilimanjaro - Picha zote na Frank Mshana










Hakuna maoni:

Chapisha Maoni