Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.
Selemani Jafo akitoa maagizo kwa Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za
Mitaa wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa Wakurugenzi wa Mamlaka
za Serikali za Mitaa leo yaliyofanyika katika ukumbi wa chuo cha
Serikali za Mitaa Hombolo, Jijini Dodoma.
Mkurugenzi
wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Dkt. Charles Mhina akiongea na
Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kwenye mafunzo ya siku mbili
kwa Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa leo yaliyofanyika
katika ukumbi wa chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Jijini Dodoma.
Baadhi
ya Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa wakimsikiliza Waziri wa
Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman
Jafo (hayupo pichani) wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa
Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa leo yaliyofanyika katika
ukumbi wa chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Jijini Dodoma.
Baadhi ya Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo (hayupo pichani) wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa leo yaliyofanyika katika ukumbi wa chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Jijini Dodoma
………………………………………..
Na. Angela Msimbira OR-TAMISEMIWaziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo ametoa wiki mbili kuanzia leo kwa Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini kuhakikisha wanabainisha maeneo ya ujenzi na mafundi watakaojenga madarasa 478 na mabweni 269.
Ameayasema hayo alipokuwa akifungua mafunzo ya siku mbili kwa Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa leo yanayofanyika katika ukumbi wa chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Jijini Dodoma.
Mhe. Jafo alisema kuwa tayari Serikali imetenga shilingi bilioni 29 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 478 mapya na Mabweni 269 ili kuhakikisha wananfunzi wote waliokosa nafasi ya kupangiwa kujiunga na kidato cha tano awamu ya kwanza wanapata katika uchaguzi wa awamu ya pili.
Mhe. Jafo amewataka Wakurugenzi hao kuhakikisha wanatumia muda mdogo kubainisha maeneo yatakayojengwa madarasa na mabweni kwa kutumia njia ya “Force Account” ili uchaguzi wa wanafunzi awamu ya pili uatakapofanyika na ujenzi huo uwe umekamilika.
Mhe. Jafo aliwaagiza Wakurugenzi hao kusimamia ujenzi huo na kuhakikisha unakamilika tarehe 30/08/2018 ili wanafunzi waliokosa nafasi ya kujiunga na Kidato cha Tano awamu ya kwanza wanachaguliwa katika awamu ya pili na kutimiza ndoto za wanafunzi hao .
Mhe Jafo aliwaagiza Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini kuhakikisha wanasimamia kwa weledi ujenzi wa miradi mbalimbali katika Halmashauri zao ikiwemo ya ujenzi wa madarasa na Mabweni ili kupunguza changamoto ya ukosefu wa madarasa nchini.
“Ninawaagiza Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Nchini kuhakikisha wanasimamia ipasavyo ujenzi wa madarasa na mabweni kwa umakini wa hali ya juu ili dhamani ya fedha inayotolewa na Serikali iendane na majengo yatakayojengwa. Alisema Jafo
Aidha Mhe. Jafo alisema sambamba na ujenzi huo Serikali imetenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya vingine 98 na kuwataka kuhakikisha wanafanyakazi kwa weledi na umakini wa hali ya juu hasa katika suala zima la usimamizi wa miradi mbalimbali ili dhamani ya fedha zinazotolewa iendane na majengo yatakayojengwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni