NAIBU WAZIRI HASUNGA AWAFUNDA WAHIFADHI WA TFS WALIOHITIMU MAFUNZO YA KIJESHI


11a
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kulia) akiwa ameongozana na kamanda wa kikosi, Simon Matura wakati  akikagua gwaride la Maafisa wa Misitu 172 kutoka Wakala wa huduma za Misitu Tanzania (TFS) na Halmashauri tano kabla  ya kuwatunuku vyeti vya kuhitimu mafunzo ya Jeshi Usu jana katika kituo cha Mlele mkoani Katavi.
2
Kamanda wa Kikosi Agness Shayo akiwa ameongoza kikosi chake kikipita  kiukakamavu mbele ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet kabla ya  kutunuku vyeti vya kuhitimu mafunzo ya Jeshi Usu jana katika kituo cha Mlele mkoani Katavi
3
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (wa tatu kushoto alieketi) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa mkoa,  Wakurugenzi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) mara baada ya kuwatunuku vyeti Maafisa misitu 172 vya kuhitimu mafunzo ya Jeshi Usu jana katika kituo cha Mlele mkoani Katavi.
4
Baadhi ya Askari wakionesha umahiri wao katika kulenga shabaha kabla ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii kuwatunuku vyeti  Wahitimu wa mafunzo ya Jeshi Usu jana katika kituo cha Mlele mkoani Katavi
5
AfisaMisitu  Mariam Kobelo akitoa salamu ya heshima kwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga kabla ya kumtunukiwa  cheti cha kuhitimu mafunzo ya Jeshi Usu yaliyofungwa jana katika kituo cha Mlele mkoani Katavi
6
Baadhi ya   Maafisa wa Misitu 172  kutoka Wakala wa huduma za Misitu Tanzania wakimsikiliza, Naibu Waziri  Japhet Hasunga muda mfupi kabla ya kutunukiwa vyeti vya kuhitimu mafunzo ya Jeshi Usu jana katika kituo cha Mlele mkoani Katavi.
7
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga  akizungumza na Maafisa wa Misitu 172 kutoka Wakala wa hudum za Misitu Tanzania (TFS) wakiwemo wa Halmashauri tano   muda mfupi kabla ya kutunukiwa vyeti vya kuhitimu mafunzo ya Jeshi Usu jana katika kituo cha Mlele mkoani Katavi
8
Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Edwin Nsoko  akizungumza na Maafisa wa Misitu 172 kutoka Wakala wa hudum za Misitu Tanzania (TFS)   muda mfupi kabla ya kutunukiwa vyeti vya kuhitimu mafunzo ya Jeshi Usu jana katika kituo cha Mlele mkoani Katavi.
9
Mwakilishi wa Mtendaji Mkuu wa TFS, Zawadi Mbwambo  akizungumza na Maafisa wa Misitu 172 kutoka Wakala wa hudum za Misitu Tanzania (TFS)   muda mfupi kabla ya kutunukiwa vyeti vya kuhitimu mafunzo ya Jeshi Usu jana katika kituo cha Mlele mkoani Katavi
10
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (katikati ) akiwa kwenye picha ya pamoja menejimenti ya   Wakala wa huduma za Misitu Tanzania (TFS) mara baada ya zoezi kuwatunuku vyeti vya kuhitimu mafunzo ya Jeshi Usu jana kumalizika katika kituo cha Mlele mkoani Katavi.
11
Baadhi ya   Maafisa wa Misitu na 172 wakiwemo kutoka Halmashauri tano wakifurahi baada ya wenzao kufanya vizuri katika ulengaji wa shabaha wakati wa   kuhitimu mafunzo ya Jeshi Usu jana katika kituo cha Mlele mkoani Katavi
12
Bendi  inayomilikiwa  Hifadhi ya Taifa (TANAPA) wakipita mbele ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japphet Hasunga wakati wahitimu wa mafunzo ya Jeshi Usu wapatao 172 walipokuwa wakimaliza mafunzo yao jana katika kituo cha Mlele mkoani Katavi
                             ( PICHA ZOTE NA LUSUNGU HELELA- MNRT
……………………
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga amewataka wahifadhi waliohitimu mafunzo ya jeshi Usu kutumia ujuzi na mbinu za kijeshi kuhakikisha wahusika wote wanaojihusisha na vitendo vya uharibifu wa misitu, wanadhibitiwa na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria bila kujenga chuki na uhasama na jamii.
Rai hiyo imetolewa kufuatia tuhuma mbalimbali kutoka kwa jamii ambazo zimekuwa zikitolewa kuvilenga  vyombo vya usalama kuwa vimekuwa mstari wa mbele kupokea rushwa, kutoa vitisho pamoja kukiuka haki za binadamu katika utendaji wao.
Alitoa rai hiyo jana alipokuwa akifunga mafunzo ya jeshi usu wilayani Mlele Katavi kwa wahitimu 172 wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania wakiwemo Maafisa Misitu waliopo Mkoani na Wilayani tisa wenye majukumu  ya kusimamia pamoja na mambo mengine Mwongozo wa Uvunaji Endelevu na Biashara ya Mazao ya Misitu.

Mhe. Hasunga aliwataka watumishi hao wajiepushe na matumizi ya nguvu yasiyo ya lazima na baadala yake watumie maarifa ya mafunzo hayo katika kuimarisha umoja na mshikamano na jamii zinazozunguka hifadhi ili wawezesha kupata taarifa  za majangili kwa urahisi.
‘’Mafunzo hayo mliyoyapa  yasiwafanye mkawa watu wa kutumia nguvu, ninawataka muwe jirani na jamii kwa kuimarisha vitengo vya kiinteligensia kuhakikisha kuwa wahusika wote wanaojihusisha na  vitendo vya uharibifu wa misitu, wanadhibitiwa na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria. Aidha, muendelee kuwa wabunifu wa mbinu za kukabiliana na uhalifu mpya unaojitokeza katika misitu yetu’’.  aliwaasa Waziri Hasunga.
Aidha, alimtaka kila mtumishi aongeze tija katika kazi zake na kuacha kufanya kazi kwa mazoea kwakuwa wameshafahamu nidhamu ya kijeshi haina lele mama. Inawezekana kila mmoja wenu atimize wajibu wake kwa wakati.
“Nimeambiwa kuwa mafunzo mliyopewa yamelenga kuongeza uwezo wenu katika kudhibiti uharibifu wa rasilimali za misitu bila kujali muda au hali . Kuna usemi usemao “A Forester must be tough and rough but not dirty “ hivyo ni imani yangu ulinzi wa misitu utaimarika kwa kiasi kikubwa kwa kuwa sasa usemi huu umetimizwa sawasawa na sio kwa maneno matupu kama mlivyozoea,” alisema Waziri Hasunga.
Kuhusu mfunzo hayo, Waziri Hasunga alisema uwepo  wa changamoto nyingi katika sekta ya maliasili, ndiko kulikoipelekea Wizara kufikia uamuzi wa kubadili utendaji wake kutoka ule wa uraia na kuwa jeshi usu. 
Kwa upande wake,Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Edwin Nsoko aliwataka wahitimu hao kufanya kazi kwa weledi pamoja  na kuzingatia miiko ya kazi yao ili misitu iendelee kuwepo kwa ajili ya kizazi cha sasa na kijacho.
Awali, Mwakilishi wa Mtendaji Mkuu wa TFS, Zawadi Mbwambo alisema mabadiliko ya mfumo wa Jeshi Usu kwa Watumishi hao umekuja muda muafaka kutokana na tatizo la ujangili wa mazao ya misitu  kuongezeka 
Aliongeza kuwa licha ya Watumishi hao kuhitimu mafunzo hayo ya Kijeshi, TFS inatumia mifumo ya kisayansi na technology katika kuratibu shughuli za usimamizi. Hivyo matumizi ya ndege zisizo na rubani (Drones) na Satelite ni kipaumbele cha Wakala na tayari matumizi ya Drones yameanza katika kusimamia misitu ya mikoko katika Delta ya Rufiji kwa kushirikiana na Shirika la Wetland International. Drones zaidi zinategemewa kuletwa nchini muda wowote kusaidia doria za mwambao wa baharí. 
Kufuatia mafunzo hayo, TFS inakuwa na jumla ya maafisa 337 waliopitia mafunzo ya jeshi usu wanaoendelea kutekeleza majukumu yao katika mfumo wa jeshi usu wakati wakisubiri Sheria na taratibu zingine.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni