Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akizungumza na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge Bungeni jijini
Dodoma, Juni 5, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akizungumza na Mbunge wa Kijitoupele Zanzibar, Shamsi Vuai Nahodha
Bungeni jijini Dodoma, Juni 5, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenyeulemavu
Jenista Mhagama, akijadili jambo na Waziri wa Elimu Profesa Joice
Ndalichako, Bungeni jijini Dodoma, Juni 5, 2018. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa, akizungumza na Waziri wa Elimu Profesa Joice Ndalichako,
Bungeni jijini Dodoma, Juni 5, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa, akisalimiana na Makamu wa Rais wa Bunge la
Afrika, Stephen Masele ambaye ni Mbunge wa Shinyanga Mjini, ofisini
kwake Bungeni mjini Dodoma, Juni 5, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa, akizungumza na Makamu wa Rais wa Bunge la
Afrika, Stephen Masele ambaye ni Mbunge wa Shinyanga Mjini, ofisini
kwake Bungeni mjini Dodoma, kutoka kushoto ni Mbunge wa Mbozi
Magharibi Mheshimiwa David Silinde na Mbunge wa Viti Maalum Zanzibar
Asha Abdullah Juma, Juni 5, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amefanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika Mheshimiwa
Stephen Masele na kumuahidi kwamba Serikali itampa ushirikiano ili aweze
kutimiza majukumu yake.
Ametoa ahadi hiyo leo (Jumanne,
Juni 5, 2018) wakati akizungumza na Mheshimiwa Masele ofisini kwake
Bungeni, Dodoma. Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kumpongeza kwa
kuchaguliwa kushika wadhifa huo.
Amesema ushindi wake katika
nafasi hiyo umelipa heshima kubwa Bunge na Serikali na kwamba wana
matarajio makubwa kwa sababu uwepo wake, utaliongezea Taifa ushirikiano
na nchi nyingine za Afrika.
“Matarajio kwa Bunge ni makubwa
kwani kuna mambo ambayo tunataka ushirikiano na nchi nyingine za
Afrika, hivyo uwepo wako ni muhimu katika kufanikisha utekelezaji wake.”
Vilevile, Waziri Mkuu
amewapongeza wabunge wengine wawili, Waheshimiwa David Silinde na Asha
Abdullah Juma kwa ushirikiano wao uliochangia ushindi wa Mheshimiwa
Masele.
Kwa upande wake, Mheshimiwa
Masele ambaye ni Mbunge wa Shinyanga Mjini, ameishukuru Serikali kwa
ushirikiano iliyompa na hatimaye kuibuka na ushindi huo.
Amesema ushindani ulikuwa mkali
kutokana na uwepo wa mataifa mengi yaliyokuwa yakiwania nafasi hiyo.
Aliahidi kutetea maslahi ya Taifa kwa muda wote atakaotumikia nafasi
hiyo. “Nakuhakikishia Waziri Mkuu kwamba nitayalinda na kuyatetea
maslahi ya Tanzania kwa muda wote ambao nitakuwa katika wadhifa huu,”
alisema Mhe. Masele.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni