Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya
Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) Dkt. Leonald Maboko, akifafanua
jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu uzinduzi wa
kampeni ya furaha ya yangu kuhamasisha huduma za kupima VVU na kuanza
ARV mapema ambayo itazinduliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Juni 19
jijini Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi wa Kinga toka
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Angela
Ramadhani akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu
uzinduzi wa kampeni ya furaha yangu ya kuhamasisha huduma za kupima VVU
na kuanza ARV mapema ambayo itazinduliwa na Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa, Juni 19 jijini Dodoma..
Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya
Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) Dkt. Leonald Maboko, akifafanua
jambo kwa waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa kampeni ya furaha yangu
kuhamasisha ya huduma za kupima VVU na kuanza ARV mapema ambayo
itazinduliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Juni 19 jijini Dodoma..
Baadhi ya washiriki wakimsikiliza
Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) Dkt.
Leonald Maboko (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa kampeni ya furaha
yangu ya kuhamasisha huduma za kupima VVU na kuanza ARV mapema ambayo
itazinduliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Juni 19 jijini Dodoma..
Naibu Mkurugenzi wa Afya toka
Shirika la Misaada la Marekani Bi. Ananthy Thambinayagan Ramadhani
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu uzinduzi wa
kampeni ya furaha yangu ya kuhamasisha huduma za kupima VVU na kuanza
ARV mapema ambayo itazinduliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Juni 19
jijini Dodoma..
Picha na Eliphace Marwa – MAELEZO, Dar es Salaam.
…………….
NA WAMJW-DAR ES SALAAM
WAZIRI Mkuu Kassim
Majaliwa,anatarajiwa kuzindua kampeni ya kitaifa ya Furaha yangu,mkoani
Dodoma Juni 19 mwaka huu,inayohusisha upimaji wa VVU na kuanza kutumia
ARV
Hayo yamezungumzwa na Kaimu
Mkurugenzi wa Huduma za Kinga Wizara ya Afya Dkt. Angera Ramadhan kuwa Kampeni hiyo imetajwa kuhamasisha mkakati wa serikali wa upimaji wa
VVU na kuanza kutumia ARV mapema kwa wale watakaokutwa na maambukizi.
“Asilimia 45 ya wanaume
wanajijua kuwa wanaishi na maambukizi ya VVU na asilimia 55 hawajijui
huku wanawake waliokuwa wanajijua kuwa wanamaambukizi ni asilimia 56 na
44 bado hawako tayari” alisema Dkt. Angera
Dkt. Angera amesema kuwa
Kuanza ARV mapema kutapunguza wingi wa VVU mwilini na kuimarisha kinga
kwa wagonjwa,hivyo kampeni hii kwa wanaume itakuwa chachu ya kujua afya
zao na wengi kuwa tayari kwa kuimarisha afya na kupunguza hatari ya
kuambukiza wenza wao.
Aidha Dkt. Angera amesema kuwa
serikali itaendelea kubuni mbinu mbadala ili kufikia malengo ya dira ya
taifa ya kutokomeza maambukizi ya Ukimwi iliyoridhia malengo ya UNAIDS
ya 90-90-90 ambayo ni kuhakikisha asilimia 90 ya watu wote wanaoishi na
VVU wanatambua afya zao,wanaanza dawa na kupunguza maambukizi mapya.
Naye Mkurugenzi wa Tume ya
Kudhibiti UKIMWI TACAIDS, Dkt. Leornad Maboko,alisema uzinduzi wa
kampeni hiyo utakuwa na siku tano za kutoa huduma za afya bila
malipo,ikiwemo upimaji wa VVU na magonjwa sugu.
Aidha Dkt. Maboko alisema
kuwa lengo la kuhamasisha kwa kauli ya Furaha yangu Pima,Jitambur
,Ishi na mwanaume njoo kwenye huduma ni kutokana na kubaini kundi hilo
kubwa halifikiwi na ili kumaliza maambukizi ni lazima kupewa hamasa.
“Hivyo tunatoa wito wakazi wa
Dodoma,mikoa ya jirani na mikoa sita ambayo ipo katika awamu ya kwanza
ya uzinduzi ikiwemo Njombe,Iringa na Mwanza kumuunga mkono Waziri Mkuu
kwa kujitokeza kwa wingi kujua afya zao na ikigundulika kutumia dawa
mapema ili kuiamrisha afya na kupunguza nguvu ya VVU,” alisema Dkt.
Maboko.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni