WATOTO WA KIKE 70 SHULE YA MSINGI ENGALAONI WILAYANI ARUSHA WAOKOLEWA NA NDOA ZA UTOTONI

Pix 1
Mkurugenzi wa Idara ya Watoto Bi. Margareth Mussai akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Engalaoni iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Arusha kuhusu madhara ya ukatili kwa watoto wakati  viongozi wa Wizara ya  na wadau wa watoto walipofika shuleni hapo kutoa elimu juu ya kujikinga na ukatili katika kuelekea maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika.
Pix 2
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Watoto kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bw. Sebastian Kitiku akiwataka wanafunzi kutumia  namba 116 kutolea taarifa kwa vitendo vya ukatili wakati  viongozi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na wadau wa watoto walipofika shuleni hapo kutoa elimu juu ya kujikinga na ukatili katika kuelekea maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika.
Pix 3
Afisa Elimu, Afya na Lishe wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha Bi. Grace Massawe akieleza jitiada za Halmashauri katika kupambana na vitendo vya ukatili kwa watoto wakati  viongozi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinisia, Wazee na Watoto na wadau wa watoto walipofika shuleni hapo kutoa elimu juu ya kujikinga na ukatili katika kuelekea maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika.
Pix 4 a Pix 4
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi wa shule ya Msingi Engalaoni iliyopo Halmshauri ya Wilaya ya Arusha wakiwasikiliza viongozi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinisia, Wazee na Watoto  na wadau wa watoto walipofika shuleni hapo kutoa elimu juu ya kujikinga na ukatili katika kuelekea maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika.
Pix 5
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Watoto kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinisia, Wazee na Watoto Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bw. Sebastian Kitiku akiimba wimbo pamoja na wanafunzi wa shule ya Msingi Engalaoni iliyopo Halmshauri ya Wilaya ya Arusha wakati viongozi wa Wizara na wadau wa watoto walipofika shuleni hapo kutoa elimu juu ya kujikinga na ukatili katika kuelekea maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika.
Picha zote na kitengo cha Mawasiliano WAMJW
………………..
Na Anthony Ishengoma WAMJW Arusha
Watoto wa kike 70 wa Shule ya Msingi Engalaoni iliyoko Kata ya Mwanditi Wilayani Arusha wameokolewa na ndoa za utotoni baada ya kuwa tayari wametolewa posa tayari kuanza maisha ya ndoa.
Hayo yamebainikiwa wakati Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali la CWDC linalojishughulisha na kupambana na ukatili kwa wanawake na watoto Bi.Hindu Mbweso akiongea na vyombo vya Habari shuleni hapo jana amesema shirika lake kwa kushirikiana uongozi wa serikali ya Mkoa wa Arusha walifanikiwa kurudisha shuleni watoto hao kwa kipindi cha mwaka 2017/18.
Aidha ameongeza kuwa sio tu watoto wa kike bali pia watoto wa kiume 12 pia walifaidika na mpango huo wa kurudishwa shuleni kwa kuwa tayari walikuwa wameachishwa Shule na familia zao ili kusaidia kuchunga ng’ombe.
Bi.Mbweso ameongeza kuwa wiki iliyopita wasichana watano wajasiri wamefanikiwa kujikomboa na ndoa za utotoni baada ya kufanikiwa kutoa taarifa kupitia dawati la jinsia la mtoto la Mkoa na tayari wanaendelea na masomo shuleni hapo huku akiwataja wengine tisa kuendelea na mpango wa MEMKWA ili kurejesha ndoto zao zizositishwa na mila potofu za Jamii ya kimasai.
Amesema katika harakati za kupambana na mimba za utotoni wazee wa kimasai wamekuwa wakiwabana kwa kuwataka watoe uhalali wa kisheria lakini tatizo hili limepatiwa ufumbuzi baada ya Wizara yenye dhamana kutoa mwongozo unaotumika kupambana na ukatili dhidi ya watoto. 
Wakati huo huo Mwenyekiti wa Kamati ya Shule hiyo Bw. Christopher Laizer amesema Jamii yake imeanza kubadili mtizamo wake dhidi ya mtoto wa kike kwani kwa sasa wameanza kujua umuhimu wa kutoa elimu kwa watoto wao.
Aidha ameongeza kuwa tatizo ni mila ambayo jamii hiyo imerithi toka kwa wazazi wao akilitaja tatizo la uelewa mdogo wa jamii yake lakini jamii hiyo imeanza kubadilika. 
Mzee huyo wa Kimasai amesema kuwa mtoto wa kike katika jamii yake amekuwa hana haki ya kusikilizwa ni kuolewa tu ili mradi mzee hata kama ana miaka 70 ametoa ng’ombe
”Mtoto wa kike kwa muda mrefu amekuwa mtaji wa kupatia ng’ombe”. Alisisitiza Mzee Laizer. 
Pamoja na Mwenyekiti wa Shule hiyo pia Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Watoto kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinisia, Wazee na Watoto Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bw. Sebastian Kitiku ameitaja namba 116 kuwa namba ya kutolea taarifa kwa vitendo vya ukatili. 
Amewataka watoto wa Shule hiyo kukalili namba hiyo ili wakipata tatizo lolote la ukatili kutoa taarifa kwa ajili ya msaada wa haraka. 
Bw. Kitiku pia atoa rai kwa Jamii ya watanzania kuzingatia Sheria ya elimu ya mwaka 2002 inayotoa adhabu ya kifungo cha miaka 30 kwa yeyote anayekatiza haki ya mtoto kujiendeleza.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni