Mkuu wa Mkoa wa Dar
es salaam Mhe. Paul Makonda leo amepokea shehena ya Vifaa vya matibabu
vyenye thamani ya shilingi milioni 100 kutoka serikali ya Korea Kusini
kupitia shirika laKOICA.
Vifaa vilivyotolewa
ni pamoja na Digital X-ray 3, Ultrasound 1, Kabati la usalama wa viumbe
(safety cabinet) 1, Mashine 3 za kupima mkojo, mashine ya kuwapa joto
watoto njiti (baby warmer) pamoja na mashine ya utakitshaji.
Baada ya kupokea
vifaa hivyo kutoka kwa Balozi wa Korea kusini Bwana Geum Young Song RC
Makonda amekabidhi vifaa hivyo kwenye vituo vya Afya vya Sinza, Mnazi
Mmoja na Mbagala ambako kuna uhaba wa vifaa.
Kabla ya kupokea
vifaa hivyo RC Makonda alifanya mazungumzo na Balozi huyo wa Korea
kusini na kuwasilisha ombi la kujengwa kwa Chuo cha kisasa cha mafunzo
ya udaktari na uuguzi ambapo Balozi Geum Young Song amepokea kwa mikono
miwili ombi hilo.
RC Makonda pia
amemueleza Balozi ombi la kujengwa kwa kituo kikubwa cha upimaji wa
magonjwa mbalimbali kwa wananchi kwenye eneo moja ambapo pia Balozi
amepokea ombi hilo na kumsifu RC Makonda kwa moyo wake wa kujali
wananchi.
Kwa upande wake
Balozi wa Korea Kusini nchini Tanzania Bwana Geum Young Song amesema
wametoa vifaa hivyo kuunga mkono kazi kubwa inayofanywa na Mkoa wa Dar
es salaam katika uboreshaji wa sekta ya Afya na wataendelea kusaidiana
na serikali.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni