Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya
pamoja na Majaji Wakuu kutoka nchi za Afrika waliohudhuria Mkutano wa
Kimataifa unaohusu Jinsia na Mahakama Afrika ulioandaliwa na Mahakama ya
Tanzania kwa kushirikiana na Benki ya Dunia na kufanyika kwenye Kituo
cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC), Wengine pichani kulia ni Jaji
Mkuu wa Ghana Sophia Akuffo,Jaji Mkuu wa Zimbabwe Luke Malaba na Jaji
Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu wengine kushoto ni Jaji Mkuu wa
Kenya David Maraga, Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Hamis Juma,
Jaji Mkuu na Jaji Mkuu wa Benin Batoko Ousmane.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Jaji Mkuu
Mstaafu Augustino Ramadhan mara baada ya kufungua Mkutano wa Kimataifa
unaohusu Jinsia na Mahakama Afrika ulioandaliwa na Mahakama ya Tanzania
kwa kushirikiana na Benki ya Dunia na kufanyika kwenye Kituo cha
Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC)
Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni