WAZEE WA MILA MARA WAENDELEA KUPINGA UKEKETAJI KWA MTOTO WA KIKE.

Na Frankius Cleophace BUTIAMA

Wazee wa Mila Muungano wa koo 12 kabila la Wakurya kwa kushirikiana na Shirika la ATFGM Masanga Tarime, wameendelea kutoa Elimu ya Kupinga suala la Ukeketaji kwa Mtoto wa kike kwa lengo la Kumnusuru ili atimize ndoto yake ya kupata Elimu na kutimiza Serikali ya Viwanda.

Wazee hao Muungano wa Koo 12 wamezungukia Koo 12 Wilayani Tarime kwa Kutoa Elimu ya kupinga Ukeketaji huku wakitoa Matamko ya Kuondoa Miiko ambayo imekuwa ikikandamiza Mtoto wa kike ambaye hajakeketwa kupitia Mikutano ya hadhara lengo  ikiwa ni kufikisha Ujumbe.

Licha ya kutoa Elimu hiyo sasa wazee hao wameamua kwenda Wilaya ya Butiama kwa lengo la kufikisha ujumbe huo uliokusudiwa, lengo ni kunusuru Mtoto wa kike.

Akitoa Elimu hiyo Mwita Nyasibora ambaye ni Katibu Msaidizi wa koo hiyo amesema kuwa ,Koo ya Bukenye ni kubwa imesambaa mpaka Wilaya ya  jirani ya Butiama, hivyo wameona ni vyema kufikisha Elimu hiyo ili wasije kukiuka na kukeketa Mtoto wa kike kwa kuwa wazee tayari wamekataa Ukeketaji.

“Sisi kama Wazee Muungano wa Koo12 tumeisha kataa Ukeketaji na Koo itakayokiuka iwajibishwe yenyewe” alisema Mwita.

Mmoja wa wazee wa Mila ametoa ushuhudi jinsi gani Mwanamke zamani alivyokuwa akinyanyaswa wakati mwingine kukeketwa wakati akijifungua jambo ambalo lilikuwa linamwongezea Uchungu mara mbili na kuendeleaza Ukatili lakini kwa sasa wazee hao wameona hakuna faida ya kukeketaji bali hasara ndo nyingi kuliko faida.

Wambura Mwema ni Mwenyekiti wa kijiji cha Buswahili Wilaya ya Butiama anasema kuwa kuna haja kubwa ya Wazee hao wa Mila kula kiapo kuhusu Matamko yao ili atakayekiuka ka kukeketa Mtoto wa kike achukuliwe hatua peke yake huku akisema kuwa Serikali inaungana na wazee hao kutokomeza Ukeketaji.

“Sasa wazee mmetamka hapa mbele yetu kuna haja kubwa ya kula kiapo ili atakayekiuka tunachukua hatua kali na serikali inapinga sana suala ili na nyie mmeongea sasa ni jukumu letu kuungana pamoja” alisema Wambura.

Licha ya kuzungumzia suala la kuipinga Ukeketaji kushirikiana na Shirika la Kupinga Ukeketaji Wilaya ya Tarime ATFGM Masanga Wazee hao wanaongeza kuwa kuna haja ya kuungana kwa pamoja sasa kukomesha suala la Wizi wa Mifugo huku wakituhumu kuwa Mifugo mingi inayoibiwa Wilaya ya Butiama inaishia Tarime.

Wazee hoa kutoka Wilaya ya Butiama wameomba Wazee wa Mila kuwa watumie mbinu ambayo walitumia Tarime na kupunguza Wizi wa Ng’ombe ili jamii iendelee kunufaika na Mifugo yao.

“Ng’ombe Wetu Wengi wanaibiwa kijijini hapa Nyao zinaishi Kijiji cha Nkerege Wilaya ya Tarime na wakati Mwingine Wilaya ya Serengeti sasa ni jukumu letu Kuungana kama Wazee na kumaliza Wizi huu” alisemaWerema Isombe Mzee wa Mila Koo ya Bukenye Butiama.

Aidha Chacha Magera ambaye ni Mwenyekiti wa Mila Koo ya Bukenye Wilayani Butiama anazidi kusisitiza suala la Amani huku Mwenyekiti wa Muungano wa Koo12 Wilaya ya Tarime Nchagwa Mtongori akisema kuwa ni jukumu la Wazee ni kurudisha heshima iliyokuwepo tangu enzi za mababu kwa kufundisha maadili mazuri likiwemo suala la Malezi na Makuzi..

Shirika la ATFGM Masanga limekuwa Mkombozi kwa watoto wa kike kioindi cha tohara uwahifadhi ili wasikeketwe mpka msimu unamalizika hivyo Serikai haina budi kuendelea kushirikiana Vyema na Shirika hilo ili Mtoto wa kike aweze kutimiza ndoto zake za Msingi ikiwemo kupata Elimu.
Picha ya Pamoja Wazee wa Mila Muungano wa Koo12 Kabila la Wakurya Wilayani Tarime Mkoani Marea na Koo ya Bukenye Wilayani Butiama baada ya kikao cha pamoja kilichofanyika kijiji cha Kongoto Kata ya Buswahili Wilayani Butiama lengo ni kuzungumzia Mikakati ya Kupiga Vita Ukeketaji kwa Mtoto wa Kike.
Katibu Msaidizi wazee wa Mila Muungano wa Koo12 ,
 
Mwita Nyasibora 
 
akitoa Elimu kwa wazee hao juu ya madhara ya Ukeketaji kwa Mtoto wa kike, ambapo amesema kuwa Wilaya ya Tarime wamezunguka na kutoa Elimu hiyo kwa jamii,hivyo wameamua kufikia Koo ya Bukenye ambayo inaenda mpaka Wilaya ya Butiama.
wazee wa Mila wakiwa katika Kikao cha pamoja
Baadhi ya Wazee wa Mila  wakiwa katika Kikao cha pamoja
 Mzee wa Mila kutoka Koo ya Bukenye Wilaya ya Butiama 
 
Werema Osombe 
 
akiomba aWazee hao kupiga Vita suala la Wizi wa Mifugo ambayo inaibiwa kutoka Wilayani humo na kupelekwa Tarime.
Mwenyekiti wa Muungano wa wazee wa Mila kabila la Wakurya Wilayani Tarime Mkoani Mara,
 
Nchagwa Mtongori 
 
 akijibu baadhi ya Maswali katika kikao hicho likiwemo suala la kutokomeza Wizi wa Mifugo na Suala la Ukeketaji kwa Mtoto wa Kike.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni