NHIF YAWAHAMAISHA WANAUSHIRIKA KUJIUNGA NA MPANGO WA BIMA YA AFYA


 
Afisa Matekelezo wa Mfuko huo mkoani Tanga Sophia Kaku
akizungumza wakati wa mkutano
wa Jukwaa la wadau wa maendeleo ya ushirika mkoani Tanga uliofanyika
kwenye ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Tanga na kufunguliwa na Katibu
Tawala wa Mkoa huo Mhandisi Zena Saidi.
MFUKO wa Taifa wa Bima
ya Afya mkoani Tanga(NHIF) umewahamasisha wanaushirika mkoani Tanga
kujiunga na mpango wa Ushirika Afya ili waweze kupata kadi za matibabu
ambazo wanaweza kunufaika na huduma ya matibabu nchini nzima kwani bila
afya imara mipango wanayopanga inaweza kushindwa kufanyika kwa ufanisi
mkubwa.
Uhamaishaji huo ulifanywa na Afisa Matekelezo wa Mfuko
huo mkoani Tanga Sophia Kaku wakati wa mkutano wa Jukwaa la wadau wa
maendeleo ya ushirika mkoani Tanga uliofanyika kwenye ukumbi wa ofisi ya
mkuu wa mkoa wa Tanga na kufunguliwa na Katibu Tawala wa Mkoa huo
Mhandisi Zena Saidi.
Alisema bila wana ushirika hao kuwa na afya
imara mipango yao wanayopanga itashindwa kufanikiwa kwa sababu
wanapokuwa wakiungua wanaweza kutumia kiasi kikubwa cha fedha nyingi
kuweza kujitibu lakini wanapokuwa kwenye mpango huo wataweza kupata
matibabu kwa gharama nafuu.
“Lakini niwaambie kuwa mkijiunga na
mpango wa ushirika mnaweza kunufaika na huduma za matibabu nchi nzima
lakini pia utawawezesha kuweza kuwa na uhakika wa matibabu wakato wote
bila kujali kama utakuwa na fedha wakati unapougua “Alisema.
Alisema
mpango wa ushirika afya ni mpango maalumu unaomuwezesha wana ushirika
kwa umoja wao kuchangia huduma za matibabu kabla ya mwanachama kupata
majanga yakiwemo maradhi,kuunguliwa au magonjwa mbalimbali wakati
wakiendelea na shughuli zao.
Hata hivyo aliwataka wanaushirika
hao kuona umuhimu wa kuwekeza kwenye mpango huo ili kuweza kupata huduma
za matibabu wakati wanapokuwa wakikumbana na maradhi mbalimbali ambayo
yanaweza kuwapelekea kushindwa kutekeleza wajibu wao kama ilivyokuwa
awali.
“Ndugu zangu niwaambieni bima ya afya ndio mambo yote
bila kuwa na afya imara mipango tunayopanga haiwezi kukamilika hivyo
niwaase tujiunge na mpango huo wa Ushirika Afya ambao ni mpango maalumu
unaowawezesha kuchangia huduma za matibabu kabla ya kupata
majanga”Alisema.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni