PROFESA WA WATOTO MUHAS ATOA MADA YA USONJI NA CHANGAMOTO YA UFAHAMU YA JAMII NA MATUNZO KWA WATOTO WENYE USONJI



Prof. Karim Manji, Profesa na Daktari Bingwa wa Watoto akitoa mada ya usonji (autism) na changamoto ya ufahamu wa jamii na matunzo ya watoto wenye usonji nchini Tanzania katika ukumbi wa mihadhara MUHAS.
Kutoka kulia mstari wa kwanza Katibu Mkuu, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Ulisubisya Mpoki, Kaimu Mkurugenzi wa Utafiti na Machapisho MUHAS, Dkt. Bruno Sunguya na Mkuu wa Skuli ya Tiba MUHAS, Prof. Sylvia Kaaya wakifuatalia mada ya usonji (autism) na changamoto ya ufahamu wa jamii na matunzo ya watoto wenye usonji nchini Tanzania katika ukumbi wa mihadhara MUHAS.
Kutoka kulia mstari wa mbele, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo – Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitafiti, Prof. Appolinary Kamuhabwa, Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. Andrea Pembe, Mwenyekiti wa mhadhara wa usonji (autism) na changamoto ya ufahamu wa jamii na matunzo ya watoto wenye usonji nchini Tanzania, Prof. Gad Kilonzo na Rais wa Jumuiya ya Alumni wa MUHAS, Prof. Charles Mgone wakifuatilia mhadhara.
Kutoka kushoto mstari w.a kwanza, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo – Mipango, Fedha na Utawala, HKMU, Prof. Ndosi na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu, NIMR, Prof. Yunus Mgaya wakimsikiliza Prof. Karim Manji akitoa mada katika ukumbi wa mihadhara MUHAS
Katibu Mkuu, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Ulisubisya Mpoki akimkabidhi zawadi Mwenyekiti wa mhadhara wa usonji (autism) na changamoto ya ufahamu wa jamii na matunzo ya watoto wenye usonji nchini Tanzania, Prof. Gad Kilonzo iliyotolewa na Idara ya Watoto MUHAS.
Prof. Karim Manji akimsaidia Mwenyekiti wa mhadhara wa usonji (autism) na changamoto ya ufahamu wa jamii na matunzo ya watoto wenye usonji nchini Tanzania, Prof. Gad Kilonzo akionyesha zawadi ya saa yenye alama (symbol) ya usonji aliyopewa.
Idara ya Watoto MUHAS wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Ulisubisya Mpoki (aliyeketi katikati), Mwenyekiti wa mhadhara wa usonji (autism), Prof. Gad Kilonzo (wa tatu kushoto), Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. Andrea Pembe (wa pili kushoto), Naibu Makamu Mkuu wa Chuo – Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitafiti, Prof. Appolinary Kamuhabwa (kushoto), Prof. Karim Manji, Profesa na Daktari Bingwa wa Watoto MUHAS (wa tatu kulia), Rais wa Jumuiya ya Alumni wa MUHAS, Prof. Charles Mgone (wa pili kulia) na Mkuu wa Skuli ya Tiba MUHAS, Prof. Sylvia Kaaya (kulia).


Na Mwandishi Wetu.
Profesa wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi Muhimbili, MUHAS ambaye pia ni Daktari Bingwa wa watoto, Prof. Karim Manji ametoa mada ya usonji (autism) na changamoto ya ufahamu wa jamii pamoja na matunzo ya watoto wenye usonji nchini Tanzania.
Mada hii ambayo aliitoa MUHAS imepata hamasa kubwa na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta ya afya ikiwa ni pamoja na Katibu Mkuu, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Ulisubisya Mpoki na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu, NIMR, Prof. Yunus Mgaya.
Akitoa mada, Prof. Manji amesema usonji ni upungufu katika ukuaji wa neva unaoathiri uwezo wa mtoto wa kuwasiliana na kujihusisha na watu wengine katika mambo mbalimbali ya kijamii. Mara nyingi upungufu huu (Usonji) huonekana kwa watoto kabla ya kufikisha miaka mitatu.
Prof. Manji ameeleza dalili mbalimbali za usonji kwa watoto ikiwa ni pamoja na mtoto kushindwa kujihusisha na watoto wenzeka, na jamii kwa ujumla na pia kuchelewa kuzungumza, hususan ikiwa ni katika kutoweza kuwasiliana. “Matamshi yanaweza kuwepo, lakini mawasiliano ni shida” Prof. Manji aliongeza.
Vile vile, ameeleza kuwa watoto wenye usonji na wazazi wao wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kunyanyapaliwa kutokana hali hiyo kutofahamika katika jamii. Profesa Manji amesema kuna ukosefu wa shule na rasilimali watu wenye ufahamu wa jinsi ya kuwatunza na kuelimisha watoto hawa ili kupunguza kasi ya matatizo ya tabia na mawasiliano.
“Tuna changamoto ya watoa huduma ya afya kwa wagonjwa wa usonji nchini, Daktari mmoja wa magonjwa ya akili anahudumia watu 300,000 na mtaalamu mmoja wa saikolojia tiba anahudumia watu 500,000” alieeleza Prof K Manji.
Kunahitaji utafiti ya hali ya juu kutafuta ufumbuzi wa chanzo ya genetic, mazingira au mambo yanoyaweza kuashiria usonji. Tunahitaji kuangalia nini tunaweza kufanya kuwasaidi watoto hawa wanaokuwa , waweze kuishi na wenzao na waweze kupata matunzo mema na kujitegemea katika jamii, Prof. Manji aliongeza.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni