Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akitazama chombo cha kupima wingi wa mvua baada ya kuzindua vituo 51 vya
kufuatilia taarifa za hali ya hewa katika viwanja vya Ofisi ya
Halmashauri ya wilaya ya Bahi mkoani Dodoma Juni 27, 2018. Wengine
pichani kutoka kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera,
Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu,Jenista Mhagama,Waziri wa
Maji, Mhandisi Isaack Kamwele, Mwakilishi Mkaazi wa Mpango wa Maendeleo
wa Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bibi Natalie Boucly na kulia ni
Mbunge wa Viti Maalum kutoka mkoa wa Dodoma, Felista Bura.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
akizindua vituo 51 vya kufuatilia taarifa za hali ya hewa katika
viwanja vya Ofisi ya Halmashauri ya wilaya ya Bahi mkoani Dodoma Juni
27, 2018. Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,
Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama. Wanne kushoto ni
Mwakilishi Mkaazi wa Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP)
nchini, Bibi Natalie Boucly.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akibonyeza kitufe wakati alipozindua vituo 51 vya kufuatilia taarifa za
hali ya hewa katika viwanja vya Ofisi ya Halmashauri ya wilaya ya Bahi
mkoani Dodoma Juni 27, 2018. K
ulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama
Baadhi ya wananchi walioshiriki
katika uzinduzi wa vituo 51 vya kufuatilia taarifa za hali ya hewa
uliofanywa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika viwanja vya Ofisi ya
Halmashauri ya wilaya ya Bahi mkoani Dodoma Juni 27, 2018.
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
………………..
WATAALAMU TUMIENI TAARIFA ZA TMA-MAJALIWA
WAZIRIMKUU Kassim Majaliwa
amewataka wataalamu wa sekta za kilimo, mifugo na maji watumie taarifa
za hali ya hewa zinazotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)
ili waongeze ufanisi katika utendaji kazi wao.
Ametoa agizo hilo leo
(Jumatano, Juni 27, 2018) wakati akizinduavituo 51 vya kufuatilia
taarifa za hali ya hewa, vituo 15 vya haidrolojia, kanzidata ya taarifa
za hali ya hewa na kituo cha operesheni na mawasiliano ya
dharura wilayani Bahi, Dodoma.
Amesemakuwa kuongezeka kwa
vituo vipya vya kisasa vya ufuatiliaji wa mwenendo wa hali ya hewa
kumeboresha uhakika wa utabiri kutoka asilimia 81 hadi 87 kama
inavyoshuhudiwa kwenye taarifa zinazotolewa katika siku za hivi
karibuni. “Hivi sasa tukiambiwa kwamba mvua itanyesha katika maeneo
fulani tunakuwa na uhakika kwa asilimia 87 ya utabiri huo,”.
“Vituo hivi ni muhimu katika
kuimarisha uwezo wa nchi wa utoaji wa huduma za hali ya hewa na
haidrolojia kwa ajili ya shughuli za maendeleo na kuongeza ufanisi
katika utoaji wa tahadhari za awali za majanga yanayosababishwa na hali
mbaya ya hewa na mabadiliko ya tabianchi,”.
Amesema kupitia mradi huo
uliofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP)
Serikali imeweza kufungua vituo 51 vya kisasa vya hali ya hewa katika
maeneo mbalimbali nchini na vituo 15 vya kupima ujazo wa maji kwenye
mito iliyopo kwenye mabonde ya Pangani, Ruvuma na Pwani ya Kusini
ambavyo vinajiendesha vyenyewe.
“Pia, mradi huu
umeiwezesha Serikali kuanzisha kanzidata ya takwimu na taarifa za
mafuriko na ukame na taarifa za hali ya hewa na kuondoa
ucheleweshwaji wa kupata takwimu au taarifa kutoka Wizara moja kwenda
Wizara nyingine,” amesema.
Hata hivyo, Waziri Mkuu
ameziagiza Wizara ya Maji na Umwagiliaji na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano zitenge fedha kwenye bajeti zao ili ziweze kufuatilia na
kusimamia mradi huo baada ya wafadhili kumaliza muda wao.
Waziri Mkuu amesema Serikali
ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli, itaendelea
kushirikiana na washirika wa maendeleo katika kuhakikisha kuwa vituo na
mifumo iliyowekwa inafanya kazi ipasavyo kwa usimamizi bora ili kufikia
malengo yaliyokusudiwa.
Uzinduzi huo umehudhuriwa na
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Vijana, Kazi, Ajira
na Wenye Ulemavu, Bibi Jenista Mhagama, Waziri wa Maji na Umwagiliaji,
Mhandisi Isack Kamwelwe na Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba.
Wengine ni Naibu Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, Naibu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Kangi
Lugola, Wabunge na Mwakilishi Mkaazi wa Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa
Mataifa (UNDP) nchini Bibi Natalie Boucly.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni