Waziri
wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isaack Kamwele akizungumza na wananchi
wa Kijiji cha Mashewa Tarafa ya Amani wilayani wakati alipofanya ziara
ya kutembelea maeneo hayo
MKUU
wa mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza katika ziara hiyo ya
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe kulia wilayani
Muheza
Kaimu
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga
Mhandisi Aram Phares akiwapungia mkono wananchi kwenye ziara hiyo
Waziri
wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe kushoto akiwa na Mkuu wa
Mkoa wa Tanga Martine Shigella wakitazama namna maji yanavyotoka kwenye
Kijiji cha Mashewa Tarafa ya Amani wakati alipofanya ziara kutembelea
vyanzo vya maji kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha
Tumbo kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga (RAS) Mhandisi Zena Saidi
Mkuu
wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga Mhandisi Mwanasha Tumbo kulia
akimueleza jambo Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe
kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigella na Katibu Tawala wa
Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe katika akisisitiza jambo kwa Katibu Tawala wa mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi wakati alipotembelea eneo la Ngomeni kwenye na
kuangalia tanki kubwa la maji ambalo litakalokuwa la lita milioni
saba linalotarajiwa kukamilika mwezi wa tatu mwakani litakuwa
limekamilika kwa ajili ya kutoa maji Pongwe Jijini Tanga hadi wilayani
Muheza kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigella
Mkandarasi
anayetekeleza mradi wa maji kutoka Pongwe hadi Jijini Tanga kutoka
kampuni ya Koberg Contrustion Co.Limited Stephen Kingili wa pili kulia
akimuonyesha jambo Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe
kushoto wakati alipotembelea na kuangalia tanki kubwa la maji eneo la
Ngomeni wilayani Muheza ambalo litakalokuwa la lita milioni
saba linalotarajiwa kukamilika mwezi wa tatu mwakani litakuwa
limekamilika kwa ajili ya kutoa maji Pongwe Jijini Tanga hadi wilayani
Muheza
Waziri
wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe akisisitiza kulia ni
Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi kushoto ni Mkuu wa
mkoa wa Tanga Martine Shigella
Waziri
wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe akiangalia mchanga
unazotumika kwenye ujenzi wa tanki la maji eneo la Ngomeni
Waziri
wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe akiangalia kikoto
zinazotumika kwenye ujenzi wa tanki la maji eneo la Ngomeni.
Mkandarasi
anayetekeleza mradi wa maji kutoka Pongwe hadi Jijini Tanga kutoka
kampuni ya Koberg Contrustion Co.Limited Stephen Kingili kulia
akizungumza na Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe
wakati alipotembelea na kuangalia tanki kubwa la maji eneo la Ngomeni
wilayani Muheza ambalo litakalokuwa la lita milioni
saba linalotarajiwa kukamilika mwezi wa tatu mwakani litakuwa
limekamilika kwa ajili ya kutoa maji Pongwe Jijini Tanga hadi wilayani
Muheza kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigella
Mkandarasi
anayetekeleza mradi wa maji kutoka Pongwe hadi Jijini Tanga kutoka
kampuni ya Koberg Contrustion Co.Limited Stephen Kingili wa pili kulia
akimuonyesha jambo Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe
kushoto wakati alipotembelea na kuangalia tanki kubwa la maji eneo la
Ngomeni wilayani Muheza ambalo litakalokuwa la lita milioni
saba linalotarajiwa kukamilika mwezi wa tatu mwakani litakuwa
limekamilika kwa ajili ya kutoa maji Pongwe Jijini Tanga hadi wilayani
Muheza
SERIKALI
imeanza kulishughulikia tatizo la maji wilayani Muheza kwa vitendo
baada ya kutoa kiasi cha bilioni 40 kwa ajili ya kutoa maji kwenye
chanzo cha mto zigi kupelekwa kwenye vijiji mbalimbali ili kuweza
kuondosha kero hizo iliyokuwepo muda mrefu iliyokuwa ikiwafanya wananchi
kutumia muda mwingi kusaka huduma hiyo.
Hayo
yalibainishwa na Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isaack Kamwele
wakati alipofanya ziara wilayani humo kutembelea vyanzo vya maji Amani
na kuzungumza na wananchi katika Kijiji cha Mashewa Tarafa ya Amani.
Alisema
kuwa mpango huo wa serikali unakusudia kuhakikisha changamoto za maji
ambazo walikuwa wanakabiliana nazo wananchi hao kwa muda mrefu
zinamaliza ili waweze kunufaika na huduma hiyo muhimu kwa ustawi wa
maisha yao na jamii zinazowazunguka.
Waziri
Kamwelwe alisema hatua hiyo ni juhudi kubwa zinazofanywa na Rais John
Magufuli kushughulikia changamoto zinazowakabili wananchi zikiwemo za
maji ili kuhakikisha tatizo la kutokupatikana kwa huduma hiyo linaondoka
kwa watanzania.
“Ndugu
zangu serikali tumetoa bilioni 40 kwa ajili ya kushughulikia tatizo la
maji wilayani Muheza kutoka chanzo cha Mto zigi kupita vijiji vyote hadi
Muheza mjini huu ni mpango wa kuhakikisha changamoto ya upatikanaji wa
huduma ya maji Muheza tunaipatia ufumbuzi wa kina “Alisema.
Aidha
alisema kutokana na juhudi kubwa zinazofanywa na Rais Dkt John Magufuli
zimeweza kuleta mafanikio ambapo juzi tumesaidia mkataba na serikali ya
India wa dola Bilioni 500 kwa ajili ya kutatua changamoto za upatikanaji
wa maji ambapo katika fedha hizo dola milioni 100 zitakuja wilaya za
Muheza na Korogwe kwa lengo la kuhakikisha wanashughulikia tatizo la
maji
“Ndugu
zangu mbunge wenu anafanya kazi kubwa na nzuri sana wakati ofisi ipo
pale Jijini Dar es Salaam alinifuata ofisini akaniambia kwenye Jimbo
lake kuna tatizo kubwa la maji hasa nyakati za kiangazi kwa wananchi
kununua maji ndoo hadi kiasi cha sh.2000 nikachukua maamuzi ya haraka
kwa lengo la kulishughulikia “Alisema.
Alisema
kuwa sio muda mrefu serikali itawapeleka wataalamu kwenye maeneo yenu
hivyo kuwataka kushirikiana nao wakati wakitekeleza shughuli zao ili
kuona namna nzuri ya kuweza kuzipatia ufumbuzi changamoto ambazo za
kutokupatikana kwa huduma kwa vijiji visivyo na uhakika wa maji.
Waziri
huyo alisema kuwa mpango wa serikali ni kuhakikisha mpaka ifikapo mwaka
2020 vijiji vyote vinakuwa na uwezo wa kupata maji ili kuweza kufikia
asilimia 85 na mijini kufikia asilimia 95 Hata hivyo alisema kuwa eneo
la Ngomeni wilayani humo kutajengwa tanki kubwa la maji litakalokuwa la
lita milioni saba ambalo litakamilika mwezi wa tatu mwakani litakuwa
limekamilika kwa ajili ya kutoa maji Pongwe Jijini Tanga hadi wilayani
Muheza(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni