Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof.
Adolf Mkenda, akizungumza na wajumbe (hawapo pichani) waliohudhuria
kikao baina yake, watendaji wa Kituo hicho na wafanyabiasha wanaozunguka
eneo hilo kabla ya kuanza kwa ziara ya kutembelea maeneo mbalimbali ya
kituo.Pro. Mkenda katika ziara hiyo aliambatana na Dkt.Susan Koech
Katibu Mkuu Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Maendeleo ya
Ushoroba wa Kati kutoka nchini Kenya. Wawili hao kwa pamoja sambamba
na kutembelea maeneo mbalimbali ya kituo hicho katika pande zote mbili
za Tanzania na Kenya walipata fursa ya kuongea na watendaji wanaohudumu
katika kituo hicho. Lengo la ziara hii ilikuwa nikuangalia ufanisi wa
kituo hicho katika kusaidia kurahisisha usafirishaji wa bidhaa na watu
kutika pande zote mbili za Tanzania na Kenya hivyo kurahisisha shughuli za biashara. Vilevile
ziara hii ililenga kubaini changamoto mbalimbali zinazokikabili kituo
hicho na kupelekea kushindwa kutoa huduma kwa ufanisi kwa wananchi
wanaotumia kituo hicho. Aidha Makatibu Wakuu hao wamezipongeza Mamlaka na Taasisi zote zilizopo katika kituo hicho kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kuhudumia wananchi. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni