Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma
Benki
ya NMB imetoa gawio la Sh. bilioni 10.1 kwa Serikali ambayo inamiliki
asilimia 32 ya hisa za Benki hiyo baada ya kupata faida ya Sh. bilioni
94.8 baada ya kodi kwa mwaka 2017/2018.
Tukio
hilo la kukabidhi hundi kifani ya gawio hilo limefanyika Makao Makuu ya
Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dodoma, kati ya Waziri wa Fedha na
Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango, kwa niaba ya Serikali, na Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki hiyo Ineke Bussemaker.
Dkt.
Mpango amezipongeza juhudi za watendaji wa Benki hiyo waliofanikisha
kupatikana kwa faida iliyowezesha Serikali kupata gawio licha ya
changamoto zilizoikumba Sekta ya Benki likiwemo suala la mikopo
chechefu.
“Mikopo
chechefu imekua tatizo kwa Benki nyingi nchini hivyo ninatoa rai kwa
Benki ya NMB kuhakikisha inafuata taratibu za kukopesha na kuendelea
kusimamia vizuri wakopaji ili kuondoa tatizo la mikopo chechefu”
alieleza Dkt. Mpango.
Aidha
ameipongeza Benki hiyo kwa kutoa huduma katika Sekta ya kilimo na
kuitaka ipanue wigo zaidi na kuziwezesha sekta za uvuvi na ufugaji
kutokana na umuhimu wake katika ukuaji wa uchumi wa taifa.
Alisema
kuwa anatarajia Benki hiyo itatoa gawio zaidi mwaka ujao wa fedha na
amemwagiza Msajili wa Hazina, kuzihakiki taasisi zote ambazo Serikali
imewekeza hisa zake ili zitoe gawio lasivyo ametishia Serikali kuondoa
hisa zake kwakuwa uwekezaji huo hautakuwa na tija.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Ineke Bussemaker alieleza
kuwa licha ya Benki yake kutoa gawio hilo la shilingi bilioni 10.1 kwa
Serikali, pia inalipa kodi za Serikali vizuri ambapo katika kipindi cha
mwaka 2017/18 imetoa kodi ya shilingi bilioni 127.
Aliongeza
kuwa tangu mwaka 2014 hadi 2017 benki hiyo imetoa kodi zinazofikia
zaidi ya shilingi bilioni 460 na kwamba itaendelea kuongeza ufanisi wa
utoaji wa huduma za kibenki ili iweze kupata faida na kulipa gawio kubwa
zaidi kwa wana hisa wake ikiwemo Serikali inayomiliki silimia 31.8 ya
hisa 500.
Aidha,
amesema kuwa Benki yake imeendelea kufanya kazi kwa karibu na Sekta ya
Kilimo kwa kutoa huduma za kifedha kwa wakulima wakiwemo wakulima wa
Tumbaku na Korosho katika mikoa ya Kusini ya Lindi na Mtwara, ambapo
imefungua zaidi ya akaunti 300,000 na kuweza kukusanya zaidi ya shilingi
bilioni 250 mwezi Novemba mwaka jana.
Bi.
Bussemaker alisema kuwa Benki yake inajitahidi kuhakikisha kunakua na
huduma jumuishi za kifedha kwa wananchi kote nchini kwa kuweka Mawakala
na kuongeza Matawi ya Benki hiyo na pia kuhamasisha wananchi wafungue
Akaunti ya Benki hiyo.
Alisema
kuwa ili kufanikisha utoaji wa huduma hiyo ya kifedha kwa watanzania,
Benki hiyo imejipanga kutumia teknolojia ya kisasa ya masuala ya fedha
ambayo itarahisisha kuwafikia watu wengi ikiwemo huduma za fedha kwa
njia ya simu za mkononi.
Katika
Mwaka wa Fedha 2016/2017, Benki hiyo ilitoa gawio la shilingi bilioni
16.5 kwa Serikali, huku kukiwa na pungufu ya shilingi bilioni 6 mwaka
huu hatua iliyomlazimu Dkt. Mpango kuiagiza Benki hiyi ihakikishe
inaboresha huduma zake ili Serikali ipate gawio kubwa zaidi kwa ajili ya
kutumia fedha hizo kuwaletea wananchi maendeleo katika sekta za maji,
afya, elimu, na miundombinu mingine muhimu.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya NMB Bi. Ineke Bussemaker (kulia), akieleza kuhusu
mkakati wa Benki yake wa kuhakikisha inaongeza ufanisi na kufungua
akaunti za wateja wengi zaidi, wakati wa hafla ya kutoa gawio la Sh.
bilioni 10.1 kwa Serikali ambayo ni mwanahisa, katika ukumbi wa Wizara
ya Fedha na Mipango Jijini Dodoma.
Msajili
wa Hazina Bw. Athuman Mbuttuka (Kushoto), Kaimu Kamisha wa Sera wa
Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Benedict Mgonya (katikati) na Kamishna wa
Fedha za Nje wa Wizara hiyo Bw. John Rubuga, wakisikiliza kwa makini
maelezo ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor. Mpango
(Mb), kuhusu taasisi za fedha kutakiwa kuwafikia wafugaji na wavuvi
wakati wa kupokea gawio la Sh. bilioni 10.1 kutoka Benki ya NMB, Jijini
Dodoma.
Kaimu
Kamishna wa Sera Bw. William Mhoja (kushoto) na Kamishna Msaidizi wa
Bajeti Bw. Pius Mponzi, wakifuatilia tukio la Benki ya NMB kuipatia
Serikali inayomiliki asilimia 32 ya hisa za Benki hiyo, mgao wa Shilingi
bilioni 10.1, baada ya kupata faida katika biashara mwaka 2017.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor. Mpango (Mb) (mbele), akitoa maelekezo kwa taasisi za fedha kuzingatia kanuni za kukopesha ili kuondoa mikopo chechefu, wakati
wa hafla ya Benki ya NMB kutoa gawio la Sh. bilioni 10.1 kwa Serikali
ambayo ni mwanahisa, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini
Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor. Mpango (Mb), akitoa
maelekezo kwa Msajili wa Hazina, Bw. Athuman Mbuttuka, kuzihakiki
taasisi zote ambazo Serikali imewekeza hisa zake ili zitoe gawio kwa
Serikali, wakati wa hafla ya Benki ya NMB kutoa gawio la Sh. bilioni
10.1 kwa Serikali ambayo ni mwanahisa, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha
na Mipango, Jijini Dodoma.
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor. Mpango (Mb) (wa sita
kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Bi. Ineke Bussemaker (wa
saba kushoto) na Maafisa waandamizi kutoka Benki ya NMB na Wizara hiyo
wakiwa katika picha ya pamoja baada ya Serikali kupokea gawio la Sh.
bilioni 10.1 kutoka NMB, Jijini Dodoma.
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor. Mpango (Mb) (kushoto)
akipeana mkono na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Bi. Ineke
Bussemaker, baada ya kupokea gawio la Sh. bilioni 10.1 kutoka NMB,
katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dodoma.
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor. Mpango (Mb) (kushoto) na
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Bi. Ineke Bussemaker, wakiangalia
hundi kifani yenye thamani ya shilingi bilioni 10.1, ambayo ni gawio
lililotolewa na Benki ya NMB kwa Serikali, Jijini Dodoma.
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor. Mpango (Mb) (kushoto) na
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Bi. Ineke Bussemaker, wakipeana
mkono wakati wa makabidhiano ya hundi kifani yenye thamani ya shilingi
bilioni 10.1, ambayo ni gawio lililotolewa na Benki ya NMB kwa Serikali,
Jijini Dodoma.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni